Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAHAFALI YA KWANZA YA DARASA LA SABA NA PRE – UNIT SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA YAFANA

MAHAFALI YA KWANZA YA DARASA LA SABA NA PRE – UNIT SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA YAFANA

Leo Jumamosi Oktoba 7,2017 kumefanyika mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
………………………………………………………………………….
Mbali na kufanyika kwa mahafali hayo ya darasa la saba pia kumefanyika mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) sambamba na uzinduzi wa Bendera na Wimbo wa shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wazazi na wadau mbalimbali wa elimu alikuwa Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi”.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ilianzishwa Julai mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 12 na kwamba mwaka huu ndiyo mara yao ya kwanza kufanya mahafali wakiwa na wahitimu 35.
“Tulianza na wanafunzi 12 katika chumba cha gereji huko Mwasele,leo shule ina jumla ya wanafunzi 622,waliohitimu mwaka huu ambao tunawafanyia mahafali ni 35,hii ni hatua nzuri tunamshukuru Mungu na wazazi ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kuhakikisha shule hii inafanikiwa”,alieleza Dominic. 
Naye Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita aliipongeza bodi ya shule, walimu,wafanyakazi wa na wazazi kwa ushirikiano walionao katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inatoa elimu bora kwa wanafunzi. 
Katika hatua nyingine Mwita alisema ili kuinua kiwango cha elimu,wameanzisha ujenzi wa shule ya sekondari na wanafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanapata usajili ili shule ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwaka 2018. 
Aidha aliwaomba wazazi na wadau wa elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujenzi unaoendelea wa jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” . 
Akitoa hotuba yake,mgeni rasmi Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products aliipongeza shule hiyo kuendelea kutoa elimu bora na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia hali inayosababisha watoto wakue vyema kiakili,kimwili na kimaadili. 
“Msingi mzuri wa elimu kwa mtoto ni kuanzia shule ya msingi hivyo nawasihi wazazi kupeleka shule,serikali yetu inapigania viwanda,viwanda hivi vinahitaji rasilimali watu,lazima tuwapatie elimu hawa watoto wetu ili maarifa wanayopata wayatumie katika viwanda hivi”,aliongeza. 

About bukuku

Check Also

PICHA TUZO

TBL Yang’ara Viwanda vya kutengeneza Bia Barani Afrika

Maofisa wa viwanda vya ABInBev wakiwa wameshikilia vyeti vya tuzo walivyojishindia katika  hafla ya kutunuku …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven + 18 =