Thursday , December 14 2017

Home / MICHEZO / NI ZAMU YA WAAMUZI DARAJA I NA II ‘KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI WENYE BEJI ZA FIFA

NI ZAMU YA WAAMUZI DARAJA I NA II ‘KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI WENYE BEJI ZA FIFA

wamburavoda

Baada ya mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi wenye beji za FIFA na wale wa Daraja la Kwanza kufanyika Agosti, 2017, sasa ni zamu ya waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili.

Waamuzi wa madaraja ya Tatu na Pili kuanzia leo Alhamisi Oktoba 12, 2017 wameanza vipimo kabla ya  mitihani ya utimamu wa mwili katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Mwanza.  

Kwa wale watakaopata matokeo mazuri, watapata fursa ya kupandisha madaraja kwa mujibu wa utaratibu.

Zoezi hilo litajumuisha pia wale waamuzi wa Daraja la Kwanza walioshindwa mitihani hiyo mwezi Agosti, mwaka huu. Hivyo nao wanaruhusiwa kwenda kufanya mitihani tena.

Kituo cha Dar es Salaam kitakuwa na waamuzi wa mikoa ya Dar es Salaam yenyewe, Pwani, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe.

Kituo cha Mwanza kitakuwa na waamuzi wa mikoa ya Mwanza yenyewe, Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Arusha, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida, Manyara na Katavi.

Waamuzi wote waende kwenye vituo vyao walivyopangiwa kama ilivyoelekezwa Oktoba 12, 2017 – ni siku ya kupima afya kabla ya kuanza kwa mitihani mingine ukiwamo wa utimamu wa mwili hapo kesho.

About Alex

Check Also

DSC_0765

YANGA KUANZA NA TIMU KUTOKA SHELISHELI LIGI YA MABINGWA

  Hatimaye wapinzani wa Yanga katika Michuano ya Kimataifa wamejulikana Leo baada ya Shirikisho la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 − one =