Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / ACHENI KUTUMIA DAWA ZA MACHO KIENYEJI NA KUNUNUA MIWANI KIHOLELA BILA USHAURI WA MTAALAMU- ANNE

ACHENI KUTUMIA DAWA ZA MACHO KIENYEJI NA KUNUNUA MIWANI KIHOLELA BILA USHAURI WA MTAALAMU- ANNE

IMG_20171012_160606

Picha ya pamoja baina ya watumishi wa afya katika klinik ya macho ya AI iliyopo Loliondo Kibaha Mkoani Pwani,na wanafunzi na mwalimu waliokwenda kupatiwa huduma ya macho bure

IMG_20171012_135057

Mtaalamu wa macho wa klinik ya macho ya AI iliyopo Loliondo Kibaha,Anne Allister wakitoa huduma ya macho kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Madaraka pamoja na mtalaamu wa macho Petro Mahundi .

Picha na Mwamvua Mwinyi

…………….

Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha
MTAALAMU wa magonjwa ya macho ,Annie Allister ,kutoka klinik ya macho ya AI Eye Solution ,Loliondo Kibaha ,Mkoani Pwani ,ameiasa jamii kuacha kununua dawa na miwani ovyo bila kupata ushauri wa daktari ,ili kuepusha kuhatarisha jicho.
Aidha ameiomba wizara ya afya kutilia mkazo udhibiti wa uuzaji miwani na dawa kiholela mitaani ,na badala yake watu wajenge tabia ya kwenda kwa wataalamu husika kupata tiba sahihi.
Anne aliyasema hayo ,siku ya kuadhimisha siku ya kuona duniani ambapo mwaka huu wamelenga afya ya macho mashuleni ,kwa walimu na wanafunzi .
Pamoja na hayo ,alisema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia dawa za kienyeji ama kuelekezana kutumia dawa zisizo za kitaalamu kama kusafisha jicho kwa chumvi,maji ya betri ,majani mbalimbali jambo ambalo linachangia kuharibu macho na kusababisha upofu .
Anne aliitaka jamii ,ielewe kuwa jicho ,ni kiungo muhimu ,hatari na kinahitaji kulindwa na kama ukifanya mchezo ukalipoteza halina spea ya mbadala .
Alielezea kwamba kutokuwa na usafi,kukosa lishe bora na matumizi ya muda mrefu ya kuangalia kompyuta,simu,vumbi,kusoma muda mrefu na kunawa maji yasiyo salama husababisha pia mtoto kuugua macho kirahisi na wengine kuumiza mishipa ya kichwa.
Mtaalamu huyo wa macho alifafanua,watu milioni 285 duniani wanakadiriwa kuwa na tatizo la magonjwa ya macho yanayoweza kuzuilika,kutibika na kuponywa ambapo kati yake milioni 246 wana shida ya uoni hafifu ,mil 39 wana upofu na mil.19 sawa na asilimia 12 ni watoto .
Alisema kati yake asilimia 65 ya watu hao ni wenye miaka kuanzia 50 na wenye uwezo mdogo kimapato .
“Kutoka na takwimu hii ya kidunia mwaka huu iliyopo Yahoo. World health.org , ndio imeamua kutoa huduma bure kwa walimu na wanafunzi hawa wa shule ya Madaraka wilayani hapa ,”
“Na ni zoezi endelevu tutakalofanya mashuleni baadae ili kupata takwimu halisi ya tatizo la macho shuleni ,na hatimae halmashauri,idara ya afya ,Elimu na wizara husika ziweze kuchukua hatua kwa lengo la kuondoa tatizo macho hata mashuleni “alisema Anne.
Anne alisema hatua kama hizo zitasaidia kutokomeza upofu unaoweza kuzuilika ifikapo 2020 kwenye maeneo yote.
Alisema endapo mwalimu haoni vizuri ,hatoweza kufundisha kwa molari ama kuwa na muda wa kumkosoa mwanafunzi ,na mwanafunzi akiwa na tatizo la macho hatoweza kusoma na atashindwa kufaulu .
Anne aliwasihi wazazi na walezi kuchukua hatua ya kuwawahisha watoto wao kwenye tiba mara wanapowaona wanalalamika shida ya macho kabla ya ugonjwa haujakomaa.
” Mtoto akiletwa kwa wataalamu mapema atapewa miwani ,au tiba inayomstahili wakati hata bado mishipa yake haijakomaa ,ikiwa miteke ,na itakuwa rahisi kutibiwa na kupona “alisema Anne .
Nae Mtaalamu wa macho ,Petro Mahundi ,alisema kati ya wanafunzi waliowapatia tiba wengi wao walikutwa na tatizo la kutoona mbali na allergy hasa ya vumbi na maji yasiyo salama.
Aliiomba jamii ,kuwa karibu na watoto wao kwa kuzingatia kuwasimamia lishe bora,usafi wa mwili na kuacha kuchezea simu na kompyuta muda mwingi na vumbi.
Kwa upande wake ,Mwalimu wa shule ya msingi Madaraka ,Carolina Daudi ,alishukuru kwa klinik ya AI kuwapatia huduma ya macho na kusema wapo baadhi ya wanafunzi wana tatizo la kushindwa kusoma ubaoni ,maandishi madogo na kwenye karatasi hasa za mitihani .
Alieleza wamekuwa wakikabiliana na changamoto hiyo kwa kuwaandikia wanafunzi hao karatasi za peke yao maandishi makubwa na ubaoni ili waweze kupata haki ya elimu kama wengine .

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini¬† vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 4 =