Thursday , December 14 2017

Home / SIASA / BOLIZOZO -VIONGOZI NDANI YA CCM TUFUATE MIIKO NA MAADILI YA UONGOZI

BOLIZOZO -VIONGOZI NDANI YA CCM TUFUATE MIIKO NA MAADILI YA UONGOZI

IMG_20171012_235623

Katibu muenezi CCM Bagamoyo ,John Francis Bolizozo ,wa kwanza kulia (pichani)

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

KATIBU mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Bagamoyo ,John Francis (Bolizozo),amewataka viongozi wa chama kuanzia ngazi ya chini ,kufuata maadili na miiko ya kiungozi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kukijengea sifa chama.

Aidha ameeleza CCM wilayani humo inatarajia kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa meal.Julius Nyerere tangu kufariki kwake miaka 18 iliyopita Oktoba 14, 1999 ,yatakayofanyika huko Msata jumamosi.

Bolizozo alieleza ,kuimarisha chama na kuendeleza sifa zake ni lazima viongozi waliopo wakasimamia maadili ipasavyo .

Alisema maadili na miiko hiyo imejengwa tangu enzi za mwalimu hivyo haina budi kuienzi .

Katibu mwenezi huyo aliwaasa vijana ambao ni wanachama wa CCM ,waache kurubuniwa na baadhi ya vyama pinzani badala yake wakipiganie na kukisemea chama mazuri na utekelezaji wa ilani unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Hata hivyo alisisitiza ,wazee wathaminiwe kwakuwa ndio waliokomboa nchi yetu na kututoa kwenye utumwa.

“Wapo baadhi ya vijana ambao hawajui nchi ilipotokea lakini wazee na waasisi walifanya kazi kubwa kutukomboa na kuliingiza taifa hili kwenye uhuru” alisema Bolizozo.

Bolizozo ,alisema waasisi hao akiwemo Mwl J.K .Nyerere waendelee kukumbukwa kwa juhudi walizozifanya sanjali na kutumia busara na hekima zao.

Akizungumzia kumbukumbu ya siku ya kifo cha baba wa taifa anasema ,wanaadhimisha huko Msata ,ambapo kutakuwepo waasisi na wazee mbalimbali .

“Kutatolewa matamko hasa ya wosia aliyotuachia hayati Mwl.Nyerere ikiwemo ,kujituma ,kuwa waadilifu,kuwa na mali zitakazosaidia kuinua mapato ya chama ,kuwa na umoja ,mshikamano na kuacha chuki miongoni mwetu ” alisema Bolizozo.

Nae Mzee Ally Mwandeni alisema ,wananchi wanapaswa kuilinda amani na utulivu uliopo toka enzi za Uhuru .

Alitaka vijana wapikwe kisiasa ili kuwekezwa kwa manufaa ya chama na taifa kwa miaka ijayo.

Mzee Mwandeni alisema ,kijana anaedharau wazee atambue anapotea kwani kuna ulazima wa kuiga mema ambayo waliyafanya wazee katika nchi na kuendelea kujifunza kwao.

About Alex

Check Also

w26

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFUGULI AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI MJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere na Mama …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − sixteen =