Thursday , November 23 2017

Home / MCHANGANYIKO / Meya Mwita Ashauri Vijana Wasichague kazi Za kufanya

Meya Mwita Ashauri Vijana Wasichague kazi Za kufanya

20171021_141355

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi waanzilishi wa shule ya Minazini waliojumuika pamoja kwenye mahafali hayo. Aliyevaa suti nyekundu ni Mkuu wa shule hiyo Maria Abihudi.

20171021_134601

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimkabizi cheti ya tuzo mwanafunzi anayemaliza elimu ya kidato cha nne Mwajabu Ibrahimu aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi.

20171021_130958

Wahitimu wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manspaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipokuwa akihutubia shuleni hapo.

20171021_130925

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wazazi, wanafunzi waliokuwa katika mahafali ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

20171021_120257

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na walimu hawapo pichani wa shule ya Sekondari Minazini iliyopo  Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya shule hiyo.

20171021_115522

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akishiriki zoezi la upandaji miti katika shuleni ya Sekondari Minazini iliyopo  Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kabla ya kuanza kwa  sherehe za mahafali ya shule hiyo.

…………………….

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI DAR

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya,  kutegemea ajira serikalini badala yake wawe wabunifu na kuwa tayari kufanya shughuli yoyote isipokuwa ya kiuhalifu.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati akizungumza na wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni ,Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni .

Meya Mwita ameeleza kuwa vijana wengi wanachagua kazi kwa malengo ya kusubiri ajira kutoka serikalini jambo ambalo alisema sio sawa na kwamba wanapaswa kufanya shughuli yoyote ambayo itawaingizia kipato na kuweza kuendesha maisha yao.

“ Vijana wangu tufanyeni kazi, tuache habari za kuchagua kazi ipi unataka kuifanya, kazi ni kazi tu ilimradi inakuingizia kipato cha kuendesha maisha yako, lakini msifanye zile ambazo mnajua sio halali mana vyombo vya dola vitawashugulikia” amesema Meya Mwita.

Mbali na hilo ,Meya Mwita amewapongeza walimu kutokana na kujitoa kwao kuwafundisha wanafunzi licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Amesema walimu wamekuwa na changamoto kadha wa kadha lakini bado wamekuwa wavumilivu ikiwemo  kuhakikisha  wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi, kamati za shule kutoa ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza majukumu yao.

“ Naelewa kwamba zipo changamoto nyingi zinazo wakabili, lakini bado mnafanya kazi kwa moyo mmoja, kutokana na juhudi hizo nawapongeza sana, zile changamoto ambazo ninauwezo wakuzitatua tutashirikiana” amesema.

Katika hatua nyingine Meya Mwita ameahidi kuwachimbia kisima cha maji shuleni hapo ili kuondokana na changamoto ya kutumia gharama kubwa ya kununua maji jambo ambalo alielezwa wakati wa risala iliyosomwa na wanafunzi washule hilo.

Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo Maria Abihudi amesema kuwa shule hiyo inachangamoto ya Umeme ambapo kwasasa upo katika jingo moja la walimu hivyo bado kusambazwa kwenye madarasa mengine ambapo Meya Mwita aliahidi kulishughulikia jambo hilo.

About Alex

Check Also

DSC_0298

UFUNGAJI WA MAFUNZO YA UDHIBITI USAMBAAJI MAFUTA BAHARINI WAFANYIKA ZANZIBAR

Injinia Mratibu wa maswala ya Mazingira Baharini kutoka ZMA Halfani Hamad Hassan kulia akitoa maelezo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 2 =