Thursday , February 21 2019

Home / BURUDANI / Miss Universe Tanzania kufanyika Jumamosi

Miss Universe Tanzania kufanyika Jumamosi

DSC_1028

Miss Universe wakijipodoa katika kambi yao ya SeaCliff Residence iliyopo Masaki jijini.

……………………………………………………………………..

Na  Mwandishi wetu

Mashindano ya kumsaka mrembo wa Kiss Universe Tanzania  yamepangwa kufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.

Maria amewataja mabondia hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam.

Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul.

Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya Miss Universe namba mbili wa mwaka jana, Lilian Loth katika kambi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana na Bonuzi.

“Maandalizi ya mashindano  hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff  Mduma,” alisema Maria.

Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.

“Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.

Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.

About bukuku

Check Also

vlcsnap-2019-02-18-13h52m43s557

WEMA SEPETU AFUNGULIWA RASMI NA BODI YA FILAMU

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four − 1 =