Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA SERA YA UGATUAJI MADARAKA KWA WANANCHI

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA SERA YA UGATUAJI MADARAKA KWA WANANCHI

1

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (mbele) akifungua kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya Ugatuaji wa Madaraka na mapendekezo ya awali ya Mpango wa Maboresho wa Sekta ya Umma Awamu ya Tatu. 2

Mtendaji Mkuu  wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akitoa neno la utangulizi katika kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya Ugatuaji wa Madaraka na mapendekezo ya awali ya Mpango wa Maboresho wa Sekta ya Umma Awamu ya Tatu. 3

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela(kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro wakifuatilia kikao cha kupokea taarifa ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi

4

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda wakati wa ufunguzi wa kikao. 5

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu katibu Mkuu Elimu Tixon Nzunda(kulia aliyekaa),Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Mhe. Amina Masenza,Mtendaji     Mkuu wa  Taasisi ya Uongozi Prof.Joseph Semboja wakiwa na Wakuu wa Mikoa walioshiriki kwenye kikao cha kupokea taarifa ya ugatuaji wa madaraka.

…………

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo  amesema kuwa Sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi imefanikiwa kwa kiasi kidogo hivyo tunahitaji kuiboresha zaidi ili dhana hii iweze kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika mamlaka ya Serikaliza Mitaa.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi  wa kikao cha  kupokea  taarifa  ya tathmini ya Ugatuaji wa Madaraka na Mapendekezo ya awali ya mpango wa maboresho ya sekta ya umma awamu ya tatu (PSRP III) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano  Hazina Mjini Dodoma.

Mhe.Jaffo amesema kuwa dhana ya ugatuaji wa madaraka ilianza kutekelezwa tangu mwaka 1998 lakini kwa kipindi kirefu dhana hii hajaeleweka vizuri kwa wahusika ndio maana hakuna mafanikio yaliyotarajiwa kwa kutambua hilo tumeona ni vyema tukafanya  tathmini jinsi ambavyo dhana hii inaweza kuboreshwa na kuleta mabadiliko kwa wananchi.

Amesema kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano Agenda kubwa ni kufanya mabadiliko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini mabadiliko haya yatapatikana kama watanzania kwa ujumla wetu wataielewa dhana kamili ya Ugatuaji wa Madaraka na kusimamia utekelezaji wake.

“Kuna viongozi wa ngazi mbalimbali katika Serikali ambao bado uelewa wa dhana ya ugatuaji bado ni mdogo kwani suala la ugatuaji si la mwananchi tu ila viongozi ndio tuliopewa dhamana ya kuhakikisha kwamba madaraka yanagatuliwa kwa kadiri inavyotakiwa katika kila ngazi ya jamii.

Amesema kuwa viongoozi mbalimbali wamepewa dhamana katika Wizara mbalimbali lakini inawezekana asijue nini anatakiwa kufanya katika sehemu yake ya kazi katika suala zima la ugatuaji wa madaraka jambo hili lilikuwa likileta mgongano katika utendaji kazi .

Mhe. Jaffo amewataka viongozi wanaoshiriki kikao cha kufanya tathmini   ya Ugatuaji wa madaraka  na mapendekezo ya awali  ya mpango wa maboresho wa sekta ya umma awamu ya tatu (PSRP III) kujadili kwa kina na kubainisha matatizo yaliyopo katika dhana ya ugatuaji wa madaraka ili mapendekezo watakayowalisha yaweze kuboresha zaidi Sera hii kwa manufaa mapana ya watanzania.

Amesema kuwa kila kiongozi anatakiwa kuhakikisha dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi inashuka katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa,Kata, mpaka ngazi ya mtaa ili kuleta maendeleo katika jamii; Ugatuzi ufanyike katika maeneo yote kuanzia madaraka ya kimamlaka, Kisiasa, Rasilimali zifikishwe chini kwa wananchi, mabadiliko ya kimahusiano pamoja Utawala unaoanzia kwa wananchi na ambao unazingatia mawazo na mapendekezo ya wananchi hao.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu- Elimu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Tixon Zunda amesema  kuwa lengo kuu la kufanya tathmini  ya hali ya Ugatuaji wa madaraka  nchini ni kutathmini halisi ya ugatuaji wa madaraka  ilivyotekelezwa kwa miaka iliyopita na kupokea mapendekezo ambayo yatatumika kuandaa Sera mpya ya Ugatuaji wa Madaraka  Nchini.

Amesema kuwa utafiti huo unatekelezwa  kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) ambapo Kampuni  ya “The Law and Development Partnership L.TD” imepewa jukumuikihusisha  wataalam washauri  wa ndani na nje ya nchi.

Awali akitoa neno la utangulizi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.Joseph Semboja alisema kikao hiki ni muhimu kwa ustawi wa Taifa letu na kimejumuisha baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa  Mikoa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi  za umma na binafsi.

Kikao hiki cha kupokea Taarifa ya ugatuaji wa madaraka na mapendekezo ya awali ya mpango wa maboresho wa Sekta ya Umma awamu ya Tatu umeandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.

TAMISEMI YA WANANCHI

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × one =