Friday , October 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / WILAYANI YA CHATO YATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

WILAYANI YA CHATO YATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege Chato ukiendelea.
 
Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na
Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Chato baada ya kuwasili
Wilayani Chato.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Chato pia ni waziri wa Nishati Mheshimi Dkt Medard Kalemani.

 

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku akifafanua
jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi wakati
wa ukaguzi wa ujenzi wa Uwanja wa ndege Chato alipotembelea na kujionea ujenzi katika moja kati ya  ziara yake ya kikazi Wilayani Humo.
 

 

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongoza viongozi katika ukaguzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
 
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
(PICHA NA MAGESA JUMAPILI AFISA HABARI MKOA WA GEITA)

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;}
 

Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka
Viongozi wa Serikali Wilayani Chato
kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Wilayani humo ili thamani ya fedha zinazotolewa ionekane.

 

Akizungumza baada ya kuwasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu
kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa amesema kuwa umefika wakati watendaji kuacha
tabia ya kukaa Ofisini bali waende maeneo mbalimbali ya Wilaya ambapo
kunatekelezwa miradi ili kusimamia kwa karibu miradi inayoendelea.
” Wananchi wanatakiwa
kusimamiwa ata kama fedha ni za kwao ili kuweka miradi katika ubora
unaotakiwa”Alisisitiza Lughumbi.
Aidha, alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato kuhakikisha
wananchi wanakuwa katika vikundi ili vishiriki katika ujenzi na utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji kwa kuchangia michango midogo
midogo kama vile kutafuta mawe, kokoto, mchanga.  Kazi kubwa ya Halmashauri ni kuhakikisha wahandisi
wanasaidia kupeleka michoro na kusimamia ujenzi wa miradi ya Zahanati na
madarasa katika vijiji husika.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato
kufuatilia ujenzi wa Bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Jikomboe ambalo
limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 75 ili kujiridhisha kama fedha hizo
zimetumika kama ilivyokusudiwa na kuona kama thamani yake inaonekana.
Akiwa Wilayani Chato Mheshimiwa Robert Gabriel ametembelea shule ya
Msingi Chato  na kukagua ujenzi wa vyumba
vya madarasa sita na vyoo, ujenzi wa Zahanati ya kijiji Mganza, ujenzi wa Bweni
shule ya Sekondari Zakia Meghj pamoja na Ujenzi wa Soko la dagaa Kasenda na
kuagiza takukuru kufika katika miradi hiyo ili kufuatilia matumizi ya fedha
katika miradi ya Zahanati, Bweni na madarasa.
Vilevile Mkuu wa Mkoa ametembelea ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na
kupongeza jitihada za utekelezaji wa mradi huo zinazoendelea kwa kufikia
asilimia 63. Awali Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku
alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa uwanja huo una Run way ya Kilometa 3 ambapo hadi
kukamilika mradi utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 39.

 

 

About Alex

Check Also

images

MWAKYEMBE APOKEA KWA MASIKITIKO TAARIFA YA KIFO CHA MTANGAZAJI ISAAC GAMBA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

7 + sixteen =