Thursday , November 15 2018

Home / MICHEZO / YANGA KUIFUATA SINGIDA UNITED KESHO BILA YA NYOTA WANNE

YANGA KUIFUATA SINGIDA UNITED KESHO BILA YA NYOTA WANNE

DSC_0765
 
Jumla ya wachezaji 22 na viongozi wa Benchi la Ufundi la Yanga kesho saa 11:30 alfajili wanatarajia kusafiri kwa basi kuelekea Singida kwa ajili ya kupambana na Singida United.
Timu hizo, zinatarajiwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua huko Singida katika mechi ya LigI Kuu Bara.
Yanga inatarajiwa kusafiri bila ya nyota wake muhimu wanne, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko ambao majeruhi na Juma Abdul anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Timu hiyo, ilifanya mazoezi yake ya mwisho saa 3:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi na Singida inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mholanzi, Hans Pluijm.
Katika mazoezi hayo, kocha wa timu hiyo  alionekana akiwapa mbinu mbalimbali za aina ya uchezaji ndani ya uwanja ili kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi hiyo.

Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili kutakuwa na mechi mbili, mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

About Alex

Check Also

tanfootball-20181113-0001

MBAO FC YAALIKWA KWENYE MICHUANO YA SPORTS PESA SUPER CUP

Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas akizungumzia michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − five =