Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / ROLI LASABABISHA AJALI MBAYA MKOANI KILIMANJARO

ROLI LASABABISHA AJALI MBAYA MKOANI KILIMANJARO

index

Kuna taarifa za Ajali mbaya ililyotokea muda huu maeneo ya Kikavu  karibu na Kwasadala Mkoani Kilimanjaro baada ya Roli   kubwa   lililokuwa lililokuwa likilipita  gari lingine  kukutana uso kwa uso  na Gari ndogo aina ya Noah lililokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda  Sanya juu  mkoani Humo.Inasadikika  Ajali hii  imesababisha  vifo kadhaa  na majeruhi walionusurika ni watu wanne. Hata hivyo Majina ya watu wanaosadikika kupoteza maisha hayakupatikana mara moja  tutaendelea kufuatilia taarifa hii na tutawajuza zaidi baadaye baada ya kupata taarifa zaidi kutoka vyombo vinavyohusika mkoani humo.

index1

About bukuku

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 5 =