Monday , October 22 2018

Home / MICHEZO / SENEGAL VINARA AFRIKA KATIKA ORODHA MPYA YA VIWANGO VYA FIFA

SENEGAL VINARA AFRIKA KATIKA ORODHA MPYA YA VIWANGO VYA FIFA

Senegal imepanda hadi nafasi ya 23 kutoka 32 katika orodha ya shirikisho la soka duniani Fifa mwezi Novemba.

Pia wamepanda juu ya Tunisia na Misri na kuwa taifa linaloorodheshwa katika nafasi ya kwanza Afrika.

Hatua hiyo inajiri baada ya Simba hao wa Teranga kushinda mechi mbili dhidi ya Afrika Kusini mnamo mwezi Novemba hatua iliowafanya kufuzu katika kombe la dunia mwaka ujao nchini Urusi.

Nigeria ndio inayoorodheshwa ya chini miongoni mwa mataifa yaliofuzu katika kombe la dunia katika mataifa hamsini duniani na manane kutoka Afrika.

Burkina Faso ndio waliopiga hatua kubwa barani Afrika baada ya kupanda nafasi 11 juu na kufikia nafasi ya 44 duniani na sita katika bara Afrika.

Mataifa yanayoongoza katika orodha hiyo ya Fifa duniani ni Ujerumani, Brazil, Ureno, Argentina na Ubelgiji.

  • 1.Senegal (23)
  • 2.Tunisia (27)
  • 3.Egypt (31)
  • 4.DR Congo (36)
  • 5.Morocco (40)
  • 6.Burkina Faso (44)
  • 7.Cameroon (45)
  • 8.Nigeria (50)
  • 9.Ghana (51)
  • 10.Ivory Coast (61)

About Alex

Check Also

44555555_710168226029625_4567196582511902720_n

AJIBU AISAIDIA YANGA KUITWANGA ALLIANCE FC 3-0 MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM KIKOSI cha Yanga SC kimeendelea kuwapa faraja mashabiki wake …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

thirteen + ten =