Wednesday , March 21 2018

Home / BURUDANI / WASANII 20 WAPUNGUZWA FIESTA DAR

WASANII 20 WAPUNGUZWA FIESTA DAR

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, amesema wamepunguza wasanii 20 ambao awali walipangwa kuwepo kwenye Tamasha la Tigo Fiesta linalotarajiwa kufanyika Jumamosi katika vya Viwanja Leaders Club.

Ruge ameyasema hayo leo katika kipindi cha Clouds360, ambapo amesema: ‘’Tulikaa kama kamati jana na tumeamua kuachana na suala la muda, tumeamua tukae kwenye muda tulioupanga sisi na kuhakikisha tuna ‘six hours’ za burudani ambazo zimepangwa na kupangika.”

Ruge alisema miongoni mwa wasanii walioondolewa kutokana na muda ni Lulu Diva,  ChinBeez, Bright, Mimi Mars, Zaiid na wengineo.

 

About Alex

Check Also

index

RC MAKONDA ATOA KIBALI CHA KURUHUSU WASANII KUREKODI VIDEO NA MOVIE ENEO LOLOTE WANALOTAKA ILI KUTANGAZA UTALII.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya watendaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

six + 3 =