Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / Balozi Mahiga katika Maadhimisho Siku ya Mshikamano na Wapalestina Dar

Balozi Mahiga katika Maadhimisho Siku ya Mshikamano na Wapalestina Dar

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mheshimiwa Balozi Maiga akizungumza kwenye sherehe ya Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestine, kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Towers,5 Desemba 2017.

 

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina. Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour wakiwa katika hafla hiyo.

 

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akitembelea picha za maonesho kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

 

Hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyoandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ikiendelea.

 

Wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina wakipata picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

About Alex

Check Also

IMG-20181021-WA0018

KITAME WAMTAKA DK. KAWAMBWA KUSHUGHULIKIA NA KUSIMAMIA KERO YA BARABARA KITAME -GAMA YENYE UREFU WA KM 9.5

Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, alhaj Dk.Shukuru Kawambwa akitolea ufafanuzi kero alizofikishiwa na wakazi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 + 13 =