Wednesday , October 17 2018

Home / BURUDANI / LISU KUNOGESHA TAMASHA LA UAMSHO JIJINI DAR ES SALAAM

LISU KUNOGESHA TAMASHA LA UAMSHO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Salesi Malula

Mwimbaji John lisu anatarajia kunogesha Kongamano kubwa la Uamsho linalotarajia kutikisa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake ambapo mhubiri maarufu kutoka Sweden mwinjilisti Johanes Amritizer anatarajiwa kuwa mnenaji mkuu wa kongamano hilo la uamsho ambalo waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wanatarajia kunogesha tamasha hilo.

Kongamano hilo kubwa linatarajia kuunganisha maelfu ya waumini pamoja na waimbaji  kutoka madhehebu mbalimbali katika masuala ya Injili ambapo waandaaji wakuu ni Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (Victory Christian Centre Tabernacle Mbezi A Jijini Dar es salaam).

Katika mahojiano maalumu, Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies  Of God – VVCT  Dkt. Huruma Nkone ambaye ndiye mwenyeji wa kongamano hilo la uamsho alisema wameandaa tukio hilo wakiamini kuwa uzoefu mkubwa wa mnenaji katika medani ya masuala injili utakua msaada mkubwa sana kwa jamii ya watu wote bila kujali utofauti wa imani na madhehebu yao kwani kuna hekima za kipekee ambazo mwiinjilisti Johanes ambaye anaheshimika sana ndani na nje ya Tanzania ataziachilia kwa wote ambao watahudhuria kongamano hili ambalo kwetu kama kanisa tunajivunia sana kwa kupewa heshima ya kipekee.

“Natoa wito kwa watu wote wa jiji la Dar es salaam kutokosa kongamano hili la kipekee ambapo pia kutakua na maombi maalumu kwa washiriki wote na kuna Baraka za kipekee ambazo mtumishi huyu anaweza kuziachilia na ni fursa ya kipekee kuhudumiwa na mtumishi huyu wa kimataifa alisistiza.

Alisema maandalizi yote yamekamilika kongamano litaanza tarehe 8-10 december 2017 kuanzia saa 10:30 jioni katika kanisa la Victory Christian Centre, lililopo Mbezi Beach A, Mwai Kibaki road, kilimani close

 waimbaji mbalimbali maarufu kama John Lisu, Rivers of Joy Internartional, sarah Ndosi, ,na Samuel yonah,na DGC Kwaya.  

About Alex

Check Also

IMG_20181014_120922

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota Mtwara kupatikana Usiku wa Leo

Mshiriki aliyeingia wawili Bora kwenye shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota toka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × four =