Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI IMEJIPANGA KUTOKOMEZA MMEA AINA YA GUGU KAROTI KATIKA HIFADHI ZA WANYAMAPORI

SERIKALI IMEJIPANGA KUTOKOMEZA MMEA AINA YA GUGU KAROTI KATIKA HIFADHI ZA WANYAMAPORI

1

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha  wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao  300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi katika mkutano huo unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha

2

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha  wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) kwa ajili ya kubadilisha ujuzi wa tafiti unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arush

3

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikabidhiwa cheti na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof. Apolinaria Pereka cha kutambua mchango uliofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufanikisha  mkutano wa kumi na moja wa uliowakutanisha wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao  300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi  unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha

4

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga akizungumza  katika mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha  wanasayansi  wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi  ulioandaliwa na TAWIRI unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC wa jijini Arusha

5

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI),  Dkt. Simon Mduma akizungumza  katika mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha  wanasayansi  wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi  unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo  katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC wa jijini Arusha

6

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kufungua mkutano wa kumi na moja uliowakutanisha  wanasayansi wa utafiti wa wanyamapori wapatao 300 kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) kwa ajili ya kubadilisha ujuzi wa tafiti unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC wa jijini Arusha 

Picha na Lusungu Helela-MNRT

……………..

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema  Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mmea  hatari uitwao gugu karoti hauoti katika maeneo ya hifadhi  kwa kuwa una madhara makubwa kwenye malisho ya wanyamapori .

Amesema mmea huo ukiota ndani ya maeneo ya hifadhi umekuwa ukizuia uoto asili kuota na hivyo kupelekea kutoweka kwa malisho ya wanyamapori.

Amesema mmea huo ulibainika miaka tisa iliyopita na umekuwaa ukisambaa katika maeneo ya nje ya  hifadhi  na athari zake zimekuwa zikionekana wazi wazi.

Amesema baada ya matokeo ya utafiti kuhusiana na mmea huo, Serikali imeamua kuiongezea bajeti   Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)  ili  iweze kufanya tafiti zaidi kuhusiana na mmea huo.  

‘’Serikali kupitia Wizara yangu tumejipanga kuhakikisha kuwa mmea huo unatokomezwa kabisa.’’ Alisisitiza  Hasunga.

Alibainisha hayo leo mjini Arusha katika Mkutano wa  utafiti wa kisayansi uliowakutanisha Wanasayansi 300  waliofanya tafiti mbalimbali katika hifadhi za wanyamapori  na mazingira kwa ujumla wa   kutoka ndani na nje ya Tanzania.  

Mkutano huo  umeanza leo na utafanyika kwa muda wa siku tatu ambapo wanasayansi watafiti mbalimbali wataziwasilisha na kuzijadili tafiti zao zipatazo 167 katika maeneo hayo.

Aidha, Naibu Waziri Hasunga amesema mkutano huo utatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu, mawazo na pia ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo kwa wanasayansi hao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TAWIRI, Prof.  Aporinalia Pereka amesema kwa upande wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) nao tayari wameanza kufanyia utafiti  mmea huo ili usiweze kusambaa zaidi kwa kuwa una madhara kwa wanyamapori na kwa binadamu pia.

Amesema kwa upande wa binadamu mmea huo umekuwa na madhara katika ngozi na upande wa wanyamapori umekuwa ukiathiri uoto asili na hivyo kupelekea  malisho ya wanyamapori kutoweka.

Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa Bodi,Prof. Pereka ameiomba serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kutenga bajeti ya kutosha ili  Taasisi hiyo iweze kufanya tafiti nyingi zaidi katika maeneo mengi ya nchi tofauti na sasa inavyofanya.

 

About Alex

Check Also

MKUU WA WILAYA YA BABATI

MAHAFALI YA 41 SHULE YA SEKONDARI SINGE HAIJAWAHI KUTOKEA

Na John Walter-Babati Mkuu wa wilaya ya Babati  Elizabeth Kitundu,  amewataka wahitimu wa kidato cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − seven =