Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua maandalizi ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru na kusema kuwa ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

 

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamsi, Desemba 7, 2017) baada ya kupokea taarifa ya kamati ya maandalizi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

 

Waziri Mkuu alisema Kamati ya Kitaifa na Kamati ya Mkoa zimejipaga vizuri na pia akagusia kuridhishwa kwake na hatua ya kamati hizo kuwaalika wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

 

Aliwataka wanakamati hao wanahakikishe wanasimamia vizuri mapokezi ya wageni na wanazingatia ratiba. “Wananchi wakija uwanjani wakaguliwe mapema na kuingizwa uwanjani ili kuepuka usumbufu wa kukaa kwenye foleni kwa muda mreru,” alisema.

 

Mapemaakitoa taarifa ya maadalizi hayo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Bibi Jenista Mhagama alisema mbali ya gwaride la heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu, kutakuwa pia na maonesho ya halaiki ya chipukizi wa shule za sekondari za Dodoma, kwaya maalumu kutoka Kyela, wimbo maalum ulioandaliwa na wasanii wa kizazi kipya na vikundi vya ngoma kutoka Kigoma, Ruvuma na Zanzibar.

 

“Tutakuwa pia na onesho la makomandoo kuruka kutoka kwenye helikopta, ndege za kijeshi, gwaride la mkoloni, kwata la kimyakimya na onesho la askari wa usalama barabarani,” alisema.

 

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA.

ALHAMISI, DESEMBA 7, 2017    

About Alex

Check Also

MKUU WA WILAYA YA BABATI

MAHAFALI YA 41 SHULE YA SEKONDARI SINGE HAIJAWAHI KUTOKEA

Na John Walter-Babati Mkuu wa wilaya ya Babati  Elizabeth Kitundu,  amewataka wahitimu wa kidato cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 3 =