Wednesday , October 17 2018

Home / MICHEZO / Z’BAR HEROES YAIFUNDISHA SOKA KILI STARS ‘SAFARI YA KURUDI NYUMBANI YAKARIBIA’

Z’BAR HEROES YAIFUNDISHA SOKA KILI STARS ‘SAFARI YA KURUDI NYUMBANI YAKARIBIA’

Timu ya Zanzibar Heroes imeifundisha soka Kilimanjaro Stars katika Michuano ya CECAFA Challenge baada ya kuitandakia jumla ya magoli 2-1 na kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Rwanda 3-1 katika mchezo wa Kundi A uliofanyika Uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya

Katika Mchezo wa Leo Z’bar Walitawala kabisa kipindi chote cha kwanza na kuwapoteza Kill Star na katika dakika ya 28 Himid Mao Mkami  aliifunga bao  baada ya pasi ya Daniel Lyanga kufuatia wawili hao kugongeana.
Kipindi cha pili, Zanzibar Heroes waliongeza kasi ya mashambulizi hadi wakafanikiwa kupata bao la kusawazisha, lililofungwa na Kassim Suleiman Khamis dakika ya 66 aliyemlamba chenga beki Boniphace Maganga na kuingia ndani ya boksi kabla ya kufumua shuti kutokea pembezoni mwa Uwanja kushoto ambalo lilimpita kipa Aishi Manula.
Wakati Tanzania Bara wakijaribu kutafuta bao la pili, wakajikuta wanafungwa wao kwa shambulizi la kushitukizwa baada ya kiungo mkongwe, Kassim Suleiman ‘Selembe’ kumlamba chenga Maganga na kutia krosi iliyounganishwa nyavuni na Ibrahim Hamad Ahmada dakika ya 78.
Zanzibar Heroes wakapata pigo dakika ya 86 baada ya mfungaji wake wa bao la kusawazisha, Khamis kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Ibrahim Abdallah Hamad.
Tanzania Bara sasa watahitaji lazima ushindi dhidi ya Kenya na Rwanda ili kuangalia uwezekano wa kwenda Nusu Fainali, jambo ni gumu hakika.

 

 

About Alex

Check Also

TAIFA

TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA KWENDA AFCON 2019,YAIDUNGUA 2-0 CAPE VERDE

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM TANZANIA imefufua matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 5 =