Friday , October 19 2018

Home / MICHEZO / NGOMA MBICHI KWA JKU NA ZIMAMOTO MICHUANO YA CAF WAPEWA VIGOGO WA AFRIKA

NGOMA MBICHI KWA JKU NA ZIMAMOTO MICHUANO YA CAF WAPEWA VIGOGO WA AFRIKA

KIKOSI CHA ZIMAMOTO FULL NEW 2 (1)

Na Salum Vuai, ZANZIBAR
TIMU ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar itaanza na Zesco United ya Zambia katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
JKU SC wataanzia nyumbani Uwanja wa Amaan, Zanzibar kabla ya kusafiri hadi Ndola kwa mchezo wa marudiano.
Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.
Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.

Na ikivuka hatua hiyo, JKU itakutana na mshindi kati ya mwakilishi wa Benin dhiai ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Timu tano hazijapangwa katika hagtua ya awali, ambazo ni Al Ahly ya Misri, mabingwa watetezi, Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Wawakilishi wa Zanzibar katika  Kombe la Shirikisho Afrika, Zimamoto wao wataanzia nyumbani pia dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia na wakivuka hatua hiyo watakutana na Zamalek ya Misri.

About Alex

Check Also

5106590-6283685-image-a-35_1539723426666

UBELGIJI NA UHOLANZI ZATOKA SARE YA 1-1 MECHI YA KIRAFIKI

Mshambuliaji wa Uholanzi, Memphis Depay akipambana na mchezaji wa Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki usiku …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × three =