Friday , January 18 2019

Home / SIASA / KABAKA APAPATA MAPOKEZI MAKUBWA NYUMBANI, AKABIDHI KADI KWA WANACHAMA WAPYA 700 WA CCM

KABAKA APAPATA MAPOKEZI MAKUBWA NYUMBANI, AKABIDHI KADI KWA WANACHAMA WAPYA 700 WA CCM

DSC05380

Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akizungumza na wanacha wa jumuiya hiyo kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Mara.

DSC05357

NAKUKABIDHI KADI. Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akimkabidhi Agnes Omar (kulia) kadi ya uanachama wa CCM.Mwanachama huyo ni miongoni mwa wanachama wapya waliojiunga na CCM mkoani Mara hivi karibuni.
Picha zote na Baltazar Mashaka
…………….
BALTAZAR MASHAKA, MUSOMA
 
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka jana amepata mapokezi makubwa mkoani Mara alikokwenda kuwashukuru wanachama wa jumuiya hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti hivi karibuni mjini Dodoma.
Mbali na mapokezi, Mwenyekiti huyo mpya wa UWT Taifa aliyechukua nafasi ya Sophia Simba aliyefukuzwa kwa makosa ya usaliti kabla ya kuomba radhi na kurejeshwa tena chamani alikabidhi kadi kwa wanachama wapya watano kati ya 700 waliojiunga na CCM kutoka vyama mbalimbali.
Mapokezi hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara Samwel Kiboye Namba Tatu, Mwenyekiti wa UWT wa Mkoa huo Wegesa Witimu , Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mkoa wa Mara Christina Samo, wenyeviti wa CCM na UWT wa wilaya, makatibu wa CCM na wa jumuiya hiyo wilaya pamoja na wanachama kutoka wilaya zzote za mkoa huo.
Akizungumza wakati wa kuwashukuru wanachama wa UWT na CCM Kabaka alisema kuwa ushindi alioupata haukutokana na makundi bali imani waliyokuwa nayo kwake wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT Taifa wa mikoa yote.
Alisema kwa kuwa uchaguzi umekwisha ni vizuri waliokuwa wagombea kwenye uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake kuvunja makundi ili kujenga CCM imara na Tanzania mpya.
Mwenyekiti huyo wa UWT  alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi ya CCM ya Mkoa wa Mara wakati akiwasalimia wajumbe wa mkutano wa UWT wa Mkoa huo.
Alisema uchaguzi umekwisha na hivyo makundi lazima yavunje na yakiachwa yaendelee kukua yataivuruga CCM kwenye chaguzi na kueleza kuwa wakati anagombea nafasi hiyo hakuwa na makundi jambo lililomwezesha kuchaguliwa kwa kura nyingi na wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa UWT uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
Kabaka alisema hakuna uchaguzi usiokuwa na makundi na uchaguzi unapomalizika ni lazima makundi hayo yavunjwe na kubaki kundi moja tu la CCM.
“ Siri ya ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na ule wa Urais, ubunge na udiwani 2020 ni kuvunja makundi.Makundi hayafai na ushindi wangu haukutokana na makundi,” alisema  Kabaka na kuongeza:
 “Nina deni kubwa hasa kwa wanawake, mliniamini na kwa kuwa pia nilimwamini Mungu kuwa natosha nilifanikiwa kuibuka mshindi  na hivyo nawashukuru wana Mara, wana CCM kwa heshima kubwa na imani mliyonipa kwani imani huzaa imani .Niwapongeze wote mliochaguliwa kuwa wenyeviti wa UWT kwa ngazi mbalimbali na jumuiya zote za CCM,”alisema.
Alieleza kuwa hakukumbatia makundi na ndiyo maana alipata ushindi mkubwa miongoni mwa wagombea 30 waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na kuahidi kuitumikia CCM na wanawake wote.
Awali akizungumza baada ya mapokezi hayo Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara Namba Tatu aliunga mkono kuvunja makundi na kusema wanawake kura zao hazipotei kutokana na misimamo yao kwa sababu siyo waongo na ndio wanaoipenda CCM.
Wakati anawasili kwenye ofisi za CCM mwenyekiti huyo wa UWT alipata mapokezi makubwa kutoka kwa wanachama wa UWT wakiwemo viongozi na wana  CCM kutoka katika wilaya saba za Mkoa wa Mara.
Kabaka aliwasili majira ya saa 5:00 asubuhi na kulakiwa na umati wa wanawake ambapo alivishwa skafu vijana wa Green Guard kisha kusalimiana nao wana CCM hao mmoja mmoja na kisha kukabidhi kadi kwa wanachama wapya 700.
Pia viongozi mbalimbali wa UWT wa mkoa na wilaya walimwagia sifa kemkem kutokana na uongozi wake tangu akiwa mwalimu, mbunge, waziri na sasa Mwenyekiti wa UWT Taifa kuwa mchango wake hautasahaulika ndani ya chama na nje ya chama.
Kabaka mwenye familia ya mtoto mmoja wa kike baada ya mtoto mwingine wa kiume kufariki dunia miaka kadhaa iliyopita alizaliwa katika Kata ya Tegeruka Wilaya ya Musoma Vijijini (sasa Butiama).
Alisoma shule ya msingi wilayani humo kabla ya kuendelea na masomo ya sekondari, chuo na kasha kuoelewa wilayani Tarime ambapo amewahi kuwa mbunge na Waziri wa Kazi na Ajira kwenye serikali ya awamu ya tatu.

About Alex

Check Also

AAAAAAAAAAAAAA

WAPINZANI WAVUTANA MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA

Na.Alex Sonna,Dodoma Muunganiko wa Vyama vya upinzani visivyo kuwa na wabunge Bungeni vimeyataka mataifa ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two + 19 =