Friday , October 19 2018

Home / BIASHARA / Uchumi wa Nchi Uko Imara – Dkt. Hassan Abbas

Uchumi wa Nchi Uko Imara – Dkt. Hassan Abbas

dk h1

Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na waandishiwa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelezo uliopo jengo la LAPF mjini Dodoma leo wakati alipotoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu masuala ya kiuchumi kufuatia taarifa ya Shirika la Fedha Duniani IMF iliyotolewa hivi karibuni, Kushoni ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Rodney Thadeus.

dk h2

Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas wakati akizungumzanao leo mjini Dodoma.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA

……………………………………………………………………………………………..

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha Duniani  (IMF) uchumi wa nchi uko imara ukilinganisha na nchi zilizofanyiwa tathimini.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.

“Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8 takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya,” amefafanua Dkt. Abba.

Ameendelea kusema, mapato ya nchi yameongezeka kutoka Shilingi Trilioni 9.9 mwaka 2015 kufikia Shilingi Trilioni 14 mwaka 2017.

Aidha, kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.

Aidha amesema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni ya watumishi wa Serikali.

Vile vile Serikali imefanikiwa kufufua viwanda vipya 17  kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina ambavyo vilikuwa vimekufa na viwanda vingine vipya zaidi ya 500 vimeanzishwa ambavyo na kuhesabika kuwa kigezo kipya cha uchumi kutokana na kutoa ajira kwa watanzania pamoja na kulipa kodi kwa Serikali.

Msemaji wa Serikali ameeleza kuwa kwa kawaida uchumi wa nchi hausimami na kwamba kuna shughuli nyingine mpya zinaingia katika uchumi na kutumika kama kigezo cha kukua kwa uchumi.

Timu hiyo ya  wataalamu kutoka IMF iliongozwa na Bw. Mauricio Villafuerte ambapo walifanya ziara juu ya tathimini ya uchumi katika nchi Saba Afrika ikiwemo Tanzania pamoja na Msumbiji, Rwanda, Nigeria, Uganda, Senegari na Cape Verde.

About bukuku

Check Also

IMG-20181018-WA0008

Tigo Yamwaga Zawadi Kibao Kwenye Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia

Mshindi wa Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia toka Mkoa wa Tanga, William …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four + 13 =