Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / GEITA WAADHIMISHA SIKU YA MAPINDUZI KWA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE

GEITA WAADHIMISHA SIKU YA MAPINDUZI KWA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki na wananchi kukusanya mchanga wa kufyatulia tofari ambazo zinatumika kujengea shule ya Sekondari kwenye Kijiji cha Mulanda kata ya Buseresere Wilaya Chato.

 

Baadhi ya viongozi wa chama Tawala pamoja na Diwani wa Kata ya Buseresere Godfey Miti wakishiriki kwenye shughuli ya ufayatuaji matofari.

 

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji wa mchanga wa kujengea madarasa ya shule ya sekondari ambayo ni mpya.

 

Diwani wa Kata ya Buseresere,Godfrey Miti akielezea namna ambavyo wananchi wameguswa kushiriki ujenzi wa shule kijiji cha Mulanda.

 

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikusanya michango kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo ambao walikuwa wamejitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Robert Luhumbi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wakiwemo na viongozi .

Na,Joel Maduka,Chato.

 

 
Ikiwa leo
Tanzania imeadhimisha miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar ,serikali Mkoani Geita
imetumia siku hiyo kwa kushirikiana na wananchi
wa Mulanda Kata ya Buseresere kufanya shughuli za maendeleo za ujenzi wa
shule ya sekondari kijijini hapo.
 
Ujenzi huo
ambao umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi  kwa kushirikiana na wanakijiji wa kijiji
hicho umetokana na adha ambazo wamekuwa wakizipata wanafunzi ambao wanasoma
shule ya sekondari ya Buseresere ambao wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita
sita kufuata elimu.
 
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi  Diwani wa Kata ya
Buseresere,Godfrey Miti ,alisema maamuzi hayo ambayo yalichukuliwa na wananchi
yametokana na kwamba kata hiyo inawananchi wengi na kwamba shule iliyopo
ilikuwa haitosho kutokana na kwamba wanafunzi wa kidato cha kwanza  736 ambao wanatarajia kusoma kwenye shule ya
kata hali ambayo inaonesha kuwepo kwa wanafunzi wengi zaidi na kwamba
kukamilika kwa shule hiyo itasaidia kupunguza wingi wa wanafunzi kwenye shule
ya sekondari Buseresere.
 
Aidha kwa
upande wake mgeni  rasmi kwenye
maadhimisho hayo ,ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi,aliwataka
wananchi kutambua kuwa akuna mgeni ambaye anaweza kuleta maendeleo na kwamba
maendeleo yanaitaji kuwa na mapinduzi ya kifikila huku akiwashukuru wananchi
kujitoa kwenye ujenzi wa shule hiyo.
 
Mhandisi,Luhumbi
ameongezea  kuwa matarajio ni kuona
ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 kila kijiji kinakuwa na zahahati ili kuhepukana
na usumbufu wa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
 
Maadhimisho ya
miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar,
mapinduzi yaliyoshuhudia kuangushwa kwa utawala wa Sultan na familia yake
January 12 mwaka 1964.
 
 Mwaka huu yamefanyika huku Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar ikiwa imepiga hatua katika kupambana na umasikini na
kuimarisha demokrasia licha ya changamoto kadhaa za kisiasa zinazoendelea
kushuhudiwa.
 
Wazanzibari
wanaona siku hii inapaswa kutumiwa na Serikali kujitathmini kuangalia hatua
walizopiga na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili Zanzibar.
 
Zaidi ya
wanamapinduzi 800 walishiriki kwenye mapinduzi hayo yaliyoifanya Zanzibar kuwa
huru kutoka kwa utawala wa Kisultani.
Sherehe za
leo zimejumuisha vikosi vya ulinzi na usalama sambamba na maandamano ya
wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar.

 

 

About Alex

Check Also

HE3

DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kiliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − six =