Thursday , July 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / TABORA WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MAPINDUZI KWA KUPANDA MITI

TABORA WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MAPINDUZI KWA KUPANDA MITI

NA TIGANYA VINCENT

RS TABORA

12 January 2018

MKUU wa Mkoa wa Tabora aggrey Mwanri amewaongoza wakazi mkoani humo katika kuadhimisha sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuendesha zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkuu wa Mkoa alianza maadhimisho kwa kupanda miti ya matunda katika Shule ya Sekondari Ngulu Wilayani Sikonge na kuungana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kazima, Tabora Wavulana na Wasichana na watumishi wa Manispaa ya Tabora kupanda pembezoni mwa barabara ya kuelekea Itigi mkoani Singida.

Alisema kuwa wakazi wa Tabora wameamua kutumia Sherehe kwa kufanya zoezi la upandaji miti badala ya kulala majumbani kwa sababu ya kutambua umuhimu wa Mapinduzi hayo yanahimiza uhumimu wa kazi ambazo zinaleta maendeleo na manufaa kwa wananchi wengi.

“Nichukue nafasi hii kama Mkuu wa Mkoa wa Tabora kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na watu wa Zanzibar kwa kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ambao yaliondoa dhuluma na unyonyaji kutoka kwa utawala wa Kisultani”alisema Mwanri.

Alisema kuwa wakazi wanaungana nao katika siku hiyo muhimu katika kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni ishara ya kutambua umuhimu wa mapinduzi hayo kwa ajili ya maendeleo yao na Tanzania kwa ujumla na kuhakikikisha kuwa Mkoa huo unakuwa wa kijani.

Mwanri aliongeza kuwa Wakazi wa Tabora pia wanawapongeza pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika kuadhimisha siku hii muhimu.

Alisema kuwa kuwa ahadi ambayo wananchi wa Tabora wanapenda kuwapa ni kuhakikisha wanafanyakazi kwa nguvu ikiwemo kupanda miti kwa wingi ili marupu rupu ya miti hiyo iweze kuwanufaisha wakazi wa visiwani kupitia mazao ya mistu kama vile asali na  mbao.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora Robert Marwa alisema kuwa wanafunzi wa Shule hiyo wakiwemo wenye ulemavu mbalimbali wameamua kupanda kuungana na Mkuu wa Mkoa huo kupanda miti ili kuweka alama katika eneo hilo katika siku hii muhimu katika Historia ya Watanzania.

Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 la wananchi wa Zanzibar waliikata minyororo ya utawala wa kisultani na vibaraka vyao ambao  walikataa madhila makubwa ya kutawaliwa waliyotendewa na utawala wa Kisultani, wakoloni, mabwanyenye na mabepari ya kunyimwa haki zao za msingi katika kuendesha maisha yao. 

About Alex

Check Also

rpc nley

WATU 18 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA

NA TIGANYA VINCENT TABORA POLISI Mkoa wa Tabora linawashikiria watu 18 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − seven =