Friday , October 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAJIBIKENI KWA WANANCHI: DKT. NDUGULILE.

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAJIBIKENI KWA WANANCHI: DKT. NDUGULILE.

Pix 1

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo ili kuchangia azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Pix 2

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Bonifasi Kasululu akiwasilisha Taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara yake alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo ili kuchangia azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

Pix 3

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya mafuta ya kupikia wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Ndimila kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.

pix 4

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akiangalia bidhaa ya majani ya kutengeneza chai maarufu kwa jina la Mchaichai wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Victory kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

pix 5

Mwakilishi wa Ofisi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw. Yolla Ludege akitoa maelezo kuhusu taratibu za kuwakagua na kuwapa vibali wanawake wajasiliamali kutengenza bidhaa zao wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Pix 6

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Rukwa Bw. Emmanuel Makere akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananwake wajasiliamali wa Mkoa wa Rukwa kuhusu majukumu ya Shirika katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.   

Pix 7

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Rukwa Bi. Ndionusia Njuyuwi akisoma taarifa kuhusu utekelezaji wa uanzishwaji na uwezeshaji wa vikundi vya wanawake kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake(WDF).

pix 8

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akielezea maana na umuhimu wa Kikundi Mlezi kwa wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Rukwa wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Pix 9

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na wanawake wajasiliamali walioshiriki kikao cha siku moja Mkoa wa Rukwa wakati wa ziara yake iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Pix 10

Baadhi ya wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) wakati wa ziara yake kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Pix 11 a

Pix 11

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa motisha kwa Vikundi ‘walelewa’ na kuwaunganisha kwa ‘Vikundi Mlezi’ ili waweze kusaidia katika kuboresha biashara zao wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Katavi kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi na kuboresha huduma ya afya kwa wananchi.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………………………………………………………………..

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwajibika kwa kuwafata wananchi mahali walipo ili kuweza kutatua changamoto zao na kuwapa mbinu mbalimbali za kupata maendeleo katika maeneo yao.

Ameyasema hayo Mkoani Katavi wakati akiitambulisha  programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika manispaa ya Sumbawanga yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana  wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujishughulisha katika shughuli za maendeleo Afisa Maendeleo ya Jamii anawajibika kushirikiana na wananchi katika kuibua miradi na kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia fursa, mazingira, soko na weledi.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati vya uzalishaji bidhaa.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasiriamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na kiufundi.

“Niseme programu hii ni muhimu kwenu wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi  amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Bonifasi Kasululu  amesema kuwa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kumuhakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa wa Rukwa.

Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Manisapaa ya Sumbawanga Bi.Beta Kainga ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kusaidiana  katika kuanzisha na kuinuka katika biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara ya siku mbili mkoani Rukwa na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kuchangia lengo la kuwa na Tanzania ya Viwanda. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda bidhaa zetu kwa kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

About bukuku

Check Also

images

MWAKYEMBE APOKEA KWA MASIKITIKO TAARIFA YA KIFO CHA MTANGAZAJI ISAAC GAMBA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 + two =