Monday , January 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / UHAKIKI WA MALI ZA UVCCM KILIMANJARO

UHAKIKI WA MALI ZA UVCCM KILIMANJARO

IMG-20180113-WA0004

   Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Kilimanjaro ikiongozwa na Mwenyekiti IVAN SAMSON MOSHI   leo tarehe 12/01/2018 imefanya uhakiki  wa mali za UVCCM KILIMANJARO
  Kamati imebaini mambo mengi ambayo yalitokea kipindi kilichopita na Mwkt ameagiza mikataba yote ipitiwe upya haraka ili kuwezesha UVCCM  kunufaika na miradi ya Vijana tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo mambo mengi hayakuwa sawa kwa Vijana!
   Baada ya uhakiki ambapo kikao kimechukuwa kutwa nzima wapo wapangaji ambao wameonekana kuwa na mapungufu makubwa katika mikataba yao Mwkt ameunda Kamati ya wajumbe wanne ambao wanafuatilia uhalali wa wao kuwa eneo la Vijana bila taarifa rasmi
   Walioteuliwa katika kamati hiyo ni ABDULRAHIM HAMADI  Katibu wa Vijana Mkoa Kilimanjaro,  YONA MAKWAIA  mjumbe kamati ya utekelezaji Mkoa,  NICE MUNICY Mjumbe Baraza Kuu Taifa,  DICKSON JONATHAN TARIMO Katibu wa UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA WA  KILIMANJARO, Aidha kamati hiyo ndogo imepewa muda wa siku Tatu kumaliza uchunguzi huo na kuleta taarifa mbele ya Kamati Utekelezaji Mkoa!

IMETOLEWA NA DICKSON TARIMO  KATIBU UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA KILIMANJARO

#KAZIINAENDELEA

About Alex

Check Also

01

WAKURUGENZI NA WAGANGA WAKUU WA HOSPITALI ZA SERIKALI JIONGEZENI BADALA YA KULALAMIKA TU

Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + six =