Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / WANANCHI MKOANI MARA WAITIKIA WITO WA MKUU WA MKOA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

WANANCHI MKOANI MARA WAITIKIA WITO WA MKUU WA MKOA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

IMG_8027

Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

IMG_8028

Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

IMG_8029

Wakazi wa kata ya Bukima Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara,  wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya Taifa.

IMG_8030

Mwenyekiti wa kijiji cha Bukima Ndg. Murungu Murungu akiwasaidia wananchi kujaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi la Usajili likiendelea kwenye ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.

IMG_8032 IMG_8034

Pichani ni Bw. Shukrani Kwikalya Mgane mkazi wa kata ya Bukima, akikamilisha hatua ya upigaji wa picha wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa. Kulia ni afisa Usajili wa  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bw. Jackson Paulo.

IMG_8035

IMG_8038

Baadhi ya Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la kuwasajili wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini wakati wa zoezi la undikishaji Vitambulisho vya Taifa katika kituo cha ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.

IMG_8039

Afisa Mtendaji Kata ya Bukima Bw. Peter Magose akikagua fomu za baadhi ya wananchi waliojitokeza kujisajili kwenye zoezi linaloendelea la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa wilaya ya Musoma Vijijini.

IMG_8046

Baadhi ya Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la kuwasajili wananchi wa kata ya Bukima wilaya ya Musoma Vijijini wakati wa zoezi la undikishaji Vitambulisho vya Taifa katika kituo cha ofisi ya mtendaji kata ya Bukima.

……………………………………………………………………………………

Wananchi mkoani Mara wamejitokeza kwa wingi kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Kighoma Ali Malima ambaye amewataka wakazi wote wa mkoa huo kuhakikisha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa ndani ya miezi mitatu ya zoezi hilo linaloendelea katika Wilaya zote za mkoa huo.

Akizungumzia mwitikio wa wananchi katika kutekeleza agizo hilo; Afisa Usajili Wilaya ya Musoma Bi. Ohana Gerald amesema mwitikio mkubwa wa watu ndiyo umepelekea kwa Wilaya ya Musoma Manispaa; zoezi la usajili kuwa  limekamilika na sasa zoezi linaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini na tayari Kata za  Bwasi, Makojo na Bukumi zimemaliza Usajili. Kata zinazoendelea na usajili kwa sasa ni Bukima, Suguti na Rusoli.

Aidha amewataka wananchi wa kata nyingine 15 ambazo bado usajili haujaanza kuanza maandalizi na kujitokeza kwa wingi pindi zoezi litakapofika katika kata zao.

Baadhi ya wananchi wameonyesha uelewa mpana wa manufaa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa na kuishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuendesha zoezi bila kulipia gharama zozote.

Pamoja na kuisifu Serikali wamemshukuru Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima kwa kuweka msukumo mkubwa wa zoezi la Usajili kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakinyanyasika kwa kukosa utambulisho na hivyo kukosa fursa nyingi na kuwapunguzia kero na usumbufu mkubwa wanaoupata sasa katika kupata baadhi ya huduma.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inategemea kumaliza zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara mwishoni mwa mwezi Februari, 2018 na kuendelea na hatua za uchakataji wa taarifa ili kuhakikisha wananchi wote wenye sifa waliosajiliwa mkoani Mara wanapatiwa Utambulisho wa Taifa kabla ya mwezi Desemba 2018.

About bukuku

Check Also

HE3

DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kiliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi  akisalimiana na Mkuu wa Wilaya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve + 3 =