Monday , October 22 2018

Home / Uncategorized / Wananchi wa Kijiji cha Muhenda Wilayani Kilosa waiomba Serikali kuwawekea ulinzi wa kutosha kwenye mashamba yao

Wananchi wa Kijiji cha Muhenda Wilayani Kilosa waiomba Serikali kuwawekea ulinzi wa kutosha kwenye mashamba yao

DSCN8418

Wananchi wa Kijiji cha Muhenda Wilayani Kilosa wameiomba Serikali kuwawekea ulinzi wa kutosha kwenye mashamba yao ili waweze kujikita katika kilimo cha pamba kama ambavyo Serikali inahamasisha.

Ombi hilo la wananchi limetolewa Januari 10 mwaka huu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa mkutano wake na wananchi hao kwa ajili ya kuwahamasisha kulima zao la pamba zao ambalo kwa mujibu wa wataalamu wa kilimo lina tija zaidi ukilinganisha na mahindi.

Wananchi hao walimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa, wao wamehamasika kulima pamba zao ambalo walikuwa wanalima hata siku za nyuma lakini kinacchowaogopesha ni uwepo wa changamoto ya mifugo ya wafugaji ambao bado wanaingiza mifugo yao kwenye mashamba ya mazao jambo ambalo linawakatisha tamaa kulima pamba.

“Mimi sijawahi kulima pamba lakini kutokana na elimu niliyoipata hapa nimeshawishika na nitalima pamba lakini Mhe. Mkuu wa Mkoa kuna changamoto hasa hapa kikjijini suala hili litatupa hofu kwa sababu ya mifugo” alisema Mkulima mmoja Bw. Bakari Mapunda

Aidha, Bw. Mapunda aliongeza kuwa wafugaji hao waliwahi kuja kijijini kwao na silaha za jadi, kunyang’anya mifugo iliyokamatwa kwa kuhatribu mazao yao, kuvunja Ofisi ya kijiji na kumvunja kidole cha mwenyekiti wao lakini hadi leo kesi hiyo haijulikani ilipofikia.

Kutokana na tuhuma hizo Dkt. Kebwe alimemtaka Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kilosa Kuwakamata mara moja wote wanaotuhumiwa na tukio hilo kuwaweka ndani na kufungua kesi hiyo upya kwa kuwa haiwezekani mtu mmoja akaisumbua Serikali na jamii kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adamu Mgoyi amesema atahakikisha suala la usalama kwa wananchi wa Muhenda na Wilaya nzima ya Kilosa linapewa umuhimu ili wananchi  waweze kujikita kwenye maendeleo hususan kilimo cha pamba huku akiwaomba kutoa ushirikiano  kwa kamati za Ulinzi na Usalama za ngazi zote.

Akiwa Wilayani Gairo Mkuu wa Mkoa  wa Morogoro alisema wananchi wa Gairo wana bahati ya kuwa na maeneo makubwa yanayofaa kilimo cha pamba kwa kuwa wana takribani kata 18 zinafaa kwa kilimo hicho na kuwataka wachangamkie fursa hiyo.

Mkuu wa Mkoa Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na timu yake wako katika ziara ya kuhamasisha wananchi wa Mkoa wa Morogoro kulima zao la pamba ambapo hadi sasa  Wilaya Nnne zimekwisha hamasishwa kulima zao la pamba ambazo ni Wilaya za Malinyi, Ulanga, Kilosa na Gairo, huku zikiwa zimesalia wilaya mbili za Morogoro na Mvomero.

DSCN8425

About bukuku

Check Also

ase

ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO

  MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisisitiza jambo mara baada …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × four =