Monday , February 26 2018

Home / MICHEZO / SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA DKT. MWAKYEMBE

SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA DKT. MWAKYEMBE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) amewapongeza Ndg. Dotto Rangimoto na Ndg. Ali Hilal Ali kwa kushinda tuzo za mashindano ya Kimataifa ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya mwaka 2017 yanayoandaliwa na Chuo Kikuu cha Cornell nchini Marekani kwakushirikiana na Kampuni ya ALAF Ltd yaliyofanyika jana tarehe 15 Januari, 2018 mjini Newyork.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa Taifa kwa ujumla, hivyo kwa niaba ya Serikali anawapongeza sana kwakutangaza utamaduni wetu kupitia lugha ya Kiswahili na kuipeperusha bendara ya Taifa letu Kimataifa. Amesema ushindi wa Ndg. Dotto na Ndg. Ali unachagiza juhudi za Serikali za kuibidhaisha lugha ya Kiswahili.

Tuzo za Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika zenye lengo la kutambua na kukuza vipaji vya uandishi kwa lugha  za Kiafrika, kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe na kutafsiri maandishi ya lugha nyingine kwa lugha za Kiafrika zili asisiwa mwaka 2014. Tuzo hizi huandaliwa kila mwaka ambapo washiriki mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki hushiriki. Katika tuzo za mwaka 2017, Ndg. Dotto Rangimoto ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Ushairi na Ndg. Ali Hilal Ali ameshinda tuzo katika kipengele cha uandishi wa Riwaya.

Octavian F. Kimario

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

16/01/2018

About Alex

Check Also

PIX 1

FIFA KUONGEZA FEDHA ZA MAENDELEO NA KUJIENDESHA KWA SHIRIKISHO

Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 − 6 =