Wednesday , December 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

  • MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SIMU YA MKONONI NA MKOBA WENYE VITU MBALIMBALI WILAYANI NYAMAGANA.

 

 

KWAMBA TAREHE 15/01/2018 MAJIRA YA SAA 06:45HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA KASESE ULIOPO KATA YA MKOLANI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA MTAMBO ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 30 HADI 35, ASIYEFAHAMIKA MAKAZI YAKE, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUCHOMWA MOTO HADI KUFARIKI DUNIA KWA TUHUMA ZA WIZI WA SIMU YA MKONONI AINA YA HUAWEI 360 YENYE THAMANI YA TSH 70,000/=, NA MKOBA WENYE VITU MBALIMBALI, MALI ZA MWANAMKE JINA TUNALIHIFADHI, MWENYE UMRI WA MIAKA 25, WAKALA WA MABASI KATIKA STENDI YA MABASI YA NYEGEZI, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MAREHEMU AKIWA NA WENZAKE WATATU WALIKUTANA NJIANI NA MWANAMKE HUYO AKIELEKEA KAZINI KATIKA STENDI YA MABASI NYEGEZI NDIPO WALIMPORA SIMU NA MKOBA WENYE VITU MBALIMBALI ALIOKUWA AMEUBEBA KISHA WALIKIMBIA. INASEMAKANA KUWA BAADA YA MWANAMKE HUYO KUPORWA MALI ZAKE ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA KWA WATU, WATU WALIOKUWEPO KARIBU NA ENEO LA TUKIO WALIJITOKEZA KUMSAIDIA HUKU KUNDI KUBWA LA WATU WAKIWAKIMBIZA WEZI HAO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MAREHEMU KISHA WAKAMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO NA MAWE NA BAADAE KUMCHOMA MOTO HADI KUFARIKI DUNIA, HUKU WENZAKE WAWILI WAKIFANIKIWA KUKIMBIA.

WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUMUOKOA LAKINI TAYARI MAREHEMU ALIKUWA AMEFARIKI DUNIA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WOTE WALIOHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI. PIA ANAWAOMBA VIJANA HUSUSANI WALE VIBAKA KUACHA SHUGHULI HIYO MARA MOJA KWANI NI HATARI, INAWEZA KUWAPOTEZEA MAISHA KAMA YALIYOMKUTA MWENZAO, LAKINI PIA NI KOSA KISHERIA.

IMETOLEWA NA;

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

 

About Alex

Check Also

02

Wachuuzi wa Soko la Samaki Bagamoyo Wamuangukia Mbalawa

  Na.Stahmil Mohamed wachuuzi wa samaki katika soko la samaki wilayani bagamoyo wamemuomba waziri maji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven − six =