Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / ZAIDI YA WANAFUNZI ELFU SABA WAANDIKISHWA DARASA LA KWANZA GEITA MJINI HUKU TATIZO LA UHABA WA MADARASA LIKIWATESA WANAFUNZI NA WALIMU

ZAIDI YA WANAFUNZI ELFU SABA WAANDIKISHWA DARASA LA KWANZA GEITA MJINI HUKU TATIZO LA UHABA WA MADARASA LIKIWATESA WANAFUNZI NA WALIMU

Mwl
Risa Nkya akiwa darasani akiwafundisha wanafunzi wa darasa la tatu  kwenye shule ya Msingi Nyankumbu iliyopo Halmashauri ya mji wa Geita huku wanafunzi wakiwa ni wengi zaidi darasani hali ambayo imepelekea wengine kukaa chini. 

 

Nje ya shule ya Msingi Nyankumbu baadhi ya madawati yakiwa yamebebanishwa kutokana na uhaba wa madarasa Shuleni Hapo.

 

Wanafunzi wakiwa darasani katika hali ya Mlundikano mkubwa zaidi.

 

Na,Joel Maduka.Geita.

 

 
Afisa elimu
wa shule za msingi katika Halmashauri ya mji wa Geita Bw Yesse Kanyuma amesema
Idara yake imeandikisha wanafunzi 7 713 wa Darasa la kwanza.
 
Bw Kanyuma
alisema  malengo ni kuandikisha wanafunzi
10109 na kwamba anaamini malengo hayo
yatafikiwa kutokana na mwenendo wa uandikishaji.
 
“Zoezi la
uandikishwaji linaendelea kwenye halmashauri yetu na hadi sasa tuna asilimia
sabini na tisa (79%) hata hivyo bado tunamatarajio ya kuandikisha wanafuzi
wengi zaidi  kutokana na kwamba zoezi
hili linaendelea hadi mwezi March”Alisema Kanyuma
 
Hata hivyo
mtandao huu umetembelea baadhi ya shule za msingi mjini Geita na kuzungumza na
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Nyankumbu Mwl Swalala David na Mwl Mkuu wa
shule ya msingi Mbugani Florence Leonard ambao wamesema changamoto kubwa
inayowakabili ni upungufu wa vyumba vya madarasa.
 
“Nina vyumba
kumi na moja vinavyotumika lakini idadi ya wanafunzi ni zaidi ya elfu tatu na
kitu ,mwaka jana nilikuwa na watoto elfu tatu na mia tano themanini na saba
lakini vyumba ni hivyo hivyo aviongezeki kwa hiyo kilio kikubwa ni vyumba vya
madarasa imefikia hatua tumeamua kutumia baadhi ya miradi tuliyonayo ili
kujenga vyumba vitatu vya madarasa ingawa na vyenyewe havitoshi kutokana na
wengi uliopo wa wanafunzi”Alisema Mwl Swalala.
 
Aidha Mwl
Swalala ameendelea kusema pamoja na matatizo ya uhaba wa madarasa hata hivyo
bado wanakabiliwa na tatizo la madarasa kuchakaa na kutengeneza nyufa hali
ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi ambao wanasoma kwenye madarasa hayo.
 
“Kutokana na
wingi wa wanafunzi imekuwa ni kazi ngumu sana kwa mwalimu pindi anapofundisha
kumpitia kila mwanafunzi na kumuelekeza hata hivyo pamoja na changamoto hizo
walimu wameendelea kujitahidi kufundisha”Alisema Mwl Leornad
 
Hata hivyo kwa
upande wake Mwl Risa Nkya alisema idadi kubwa ya wanafunzi madarasani kumekuwa
kukiwanyima amani walimu wengi na kujikuta wakitimiza wajibu tu wakufundisha
kwani hali ya mlundikano wa wanafunzi ni kubwa sanaa.
 
Baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Nyankumbu akiwemo Devid Cosmas na Devota John
wameelezea kuwa hali ya mlundikano ni tatizo ambalo linaweza kuchangia kushusha
kiwango cha cha Elimu kwani wamekuwa wakishindwa kusoma vizuri kutokana na
wingi wa wanafunzi kwenye madarasa ambayo wanasomea hivyo wameiomba serikali
pamoja na wadau kujitoa kwa dhati kutatua kero ya uhaba wa madarasa shuleni
hapo.
 

 

 

About Alex

Check Also

index

Serikali Yawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Zote Nchini Kuhakikisha Wanatokomeza Malaria

Na, Paschal Dotto- MAELEZO 22.10.2018 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − thirteen =