Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / DKT WMIGULU NCHEMBA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA NA MADEREVA WA DALADALA JIMBONI KWAKE

DKT WMIGULU NCHEMBA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA NA MADEREVA WA DALADALA JIMBONI KWAKE

 index

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt.  Mwigulu Nchemba akiongea na vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliyopo stand kuu ya mabasi iramba kuhusu usalama wao waendeshapo pikipiki

……………………………………………………………………………..
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi  na Mbunge wa jimbo la Iramba Dkt. Mwigulu Nchemba leo amewatembelea wafanyabiashara ndogondogo katika soko kuu la wilaya ya Iramba, Madereva wa pikipiki na madereva wa daladala na makodakta waliopo stendi kuu ya mabasi Kiomboi ili kusikiliza changomoto wanazokutana nazo katika utendaji wao wa kazi za kila siku na kuwasilisha katika balaza la madiwani.

Kwa upande wa madereva wa bodaboda Dkt. Mwigulu amewashauri waendeshe bodaboda zao kwa usalama na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kukamatwa mara kwa mara na askari polisi pale wanapofanya  makosa.

Wafanyabiashara ndogondogo wa soko kuu la mji wa Kiomboi wamemuomba mbunge wao kuwasaidia kupunguza kodi nyingi ambazo wanakutana nazo wakati wanafanya biashara katika soko hilo, ombi lao limepokelewa na Dkt. Mwigulu na ameahidi kukaa nao ili kuona njia nzuri za kutatua changamoto zao.

Baraza la madiwani linatarajia kukutana  mchana  leo ambapo changamoto mbalimbali alizozipokea  ataziwakilisha kupata utatuzi katika kikao hicho.

About bukuku

Check Also

index

Serikali Yawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Zote Nchini Kuhakikisha Wanatokomeza Malaria

Na, Paschal Dotto- MAELEZO 22.10.2018 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 5 =