Monday , February 26 2018

Home / MICHEZO / LIGI DARAJA LA PILI KILIMANJARO HEROES NA AFC ZAPIGWA FAINI LAKI MBILI KILA MMOJA

LIGI DARAJA LA PILI KILIMANJARO HEROES NA AFC ZAPIGWA FAINI LAKI MBILI KILA MMOJA

African-Sports

Mechi namba 28 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 0 v Pepsi 2). Klabu ya Kilimanjaro Heroes imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.

Adhabu dhidi ya Kilimanjaro Heroes imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 30 Kundi B (African Sports 2 v AFC 0). Wachezaji wa AFC, John George Rasta na Shaibu Salim wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutaka kumshambulia Mwamuzi kabla ya kuokolewa na viongozi wa timu hiyo katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 3, 2018 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Klabu ya AFC imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(13) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

About Alex

Check Also

PIX 1

FIFA KUONGEZA FEDHA ZA MAENDELEO NA KUJIENDESHA KWA SHIRIKISHO

Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari hawapo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 − seven =