Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

msangi

  • WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 104.4, WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 12.02.2018 MAJIRA YA SAA 20:58HRS USIKU KATIKA MTAA WA KILOLELI KATA NYASAKA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHAFII ABDALLAH, MIAKA 21, MKAZI WA MTAA WA NYAMANORO NA 2. JOHN JOHN, MIAKA 19, MKAZI WA MTAA WA KITANGIRI, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 104.4, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

AWALI POLISI WAKIWA  DORIA WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU WAPO WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI. AIDHA BAADA YA POLISI  KUPOKEA TAARIFA HIZO WALIFANYA UPELELEZI NA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO NA BAADAE WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA KWANZA AITWAYE SHAFII ABDALAH AKIWA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 38 NA BAADAEA ALIKAMATWA MTUHUMIWA MWINGINE AITWAYE JOHN JOHN AKIWA NA BHANGI KIASI CHA GRAMU 66.4.

POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOSHIRIKIANA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU KATIKA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA  DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KOSA KISHERIA. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU MAPEMA ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI.

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

About Alex

Check Also

index

Serikali Yawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Zote Nchini Kuhakikisha Wanatokomeza Malaria

Na, Paschal Dotto- MAELEZO 22.10.2018 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − one =