Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / Waandishi wa Habari Watakiwa Kuzingatia Weledi

Waandishi wa Habari Watakiwa Kuzingatia Weledi

Pix 1

Mwakilishi kutoka  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) Bi. Faith Shayo akiongea wakati wa kuadhimisha siku ya Redio Duniani  leo Mkoani Dodoma, katikati nia Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge .

Pix 2

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge (wa kwanza kulia) akiongea kwa ajili ya kumkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)  katika hafla ya kuadhimisha siku ya Redio Duniani ambayo kitaifa imefanyika leo Mkoani Dodoma, kushoto ni Mwakilishi kutoka  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Kimataifa (UNESCO) Bi. Faith Shayo.

Pix 3 Pix 4

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiongea na waandishi wa habari na watangazaji wa Radio katika hafla ya kuazimisha siku ya Redio Duniani ambapo aliwataka kuzingatia maadili ya utangazaji kwa kudumisha,amani,upendo na mshikamano.

Pix 6

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walihudhuria maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika leo Mkoani Dodoma, kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge.

Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma

…………….

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili kwa kuandika habari zenye ukweli na uhakika kwa manufaa ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.

Mhe. Shonza ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Redio Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi na watangazaji wa redio za jamii kutoka mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro, Mtwara, Shinyanga, Songwe, Geita, Mwanza, Kagera, Dodoma, Pemba, Unguja, Lindi na Songwe.

“Redio za jamii zimekuwa tegemeo kubwa la kupata habari kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini hasa pembezoni mwa nchi. Mwananchi haitaji kuwa na umeme anapotaka kusikiliza Redio,” alisema Shonza.

Amesema, ni vyema waandishi wawe wa kweli wanapotoa habari mbalimbali kwa wananchi ili kuepuka machafuko ya nchi kama ilivyotokea nchini Rwanda, ambapo chanzo cha machafuko hayo kilitokana na habari zilizotangazwa kupitia Redio.

“Wananchi wanategemea habari toka kwenu ili kujua namna Serikali inavyotekeleza majukumu yake pamoja na kutatua changamoto zao,” alisema Mhe. Shonza.

Vile vile kupitia Redio za Kijamii, wananchi ambao ni wakulima wanaweza kujua maeneo yalipo masoko kwa ajili ya mazao yao.

Naye,  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge amewata waandishi wa habari kuitangaza Dodoma pamoja na fursa zilizomo mkoani humo kwa kuwa ni ya Serikali ni kuifanya Dodoma kuwa kituo cha mji wa kiuchumi.

“Mpaka sasa jumla ya watumishi 3000 wamehamia mkoani humu na kufikia Juni mwaka huu jumla ya watumishi wa Serikali 7000 watakuwa wamehamia. Hivyo fursa nyingi zitahamia mkoani humu,” alisema Dkt. Mahenge.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Faith Shayo amewataka waandishi wa habari hao kutumia vizuri vipaza sauti vyao katika kudumisha amani ya nchi, kuchochea maendeleo, kupinga unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kuweka msisitizo wa  usawa wa kijinsia.

About Alex

Check Also

index

Serikali Yawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Zote Nchini Kuhakikisha Wanatokomeza Malaria

Na, Paschal Dotto- MAELEZO 22.10.2018 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − 13 =