Monday , October 22 2018

Home / MCHANGANYIKO / TRA YAWATAKA WAFANYABIASHARA WA SONGWE KUTUMIA EFD

TRA YAWATAKA WAFANYABIASHARA WA SONGWE KUTUMIA EFD

T17-640x330

Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Charles kichere amewataka wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti za EFD kwa kuwa mashine hizo zinaweka kumbukumbu za biashara zao na kuwezesha TRA  kuwakadiria kodi stahiki isiyo na manung’uniko.

Kamishna Kichere ameyasema hayo alipozungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe akiwa katika ziara yake ya kukagua matumizi ya mashine za efd pamoja na mambo mengine katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Hali kadhalika Kamishna Kichere amewaonya wafanyabiashara wa mkoa huo kuacha kufanya udanganyifu katika kutoa risiti zenye bei pungufu kuliko kiasi cha pesa ambacho mteja amelipa kwa kuwa huo ni ukwepaji wa kodi na atakayebainika atatozwa faini kwa mujibu wa sheria za kodi.

Naye Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw.Elijah Mwandumbya amesema kwa wafanyabiashara wadogo ambao mapato yao hayazidi  shilingi milioni 20, ambao wamenunua mashine za efd hawatalipa makadirio yao ya kodi mara watakapokadiriwa na tra isipokuwa kodi ambayo watapaswa kulipa itafidia gharama ya mashine za efd.

Nao wafanyabiashara wa mkoa wa songwe wamemweleza kamishna mkuu wa tra juu ya changamoto ya kutokupata huduma kwa wakati toka kwa mawakala pindi mashine hizo zinapoleta hitilafu ambapo sheria inawataka mashine iwe imetengemaa ndani ya saa 48.

Hata hivyo, Bw Mwandumbya amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa tayari kuna mawakala wamekubali kufungua ofisi zao katika mji wa Mbozi  ili kurahisisha matengenezo ya mashine pindi zinapoleta hitilafu na hivyo changamoto hiyo kupatiwa ufumbuzi.

Mkoa wa Songwe ni mmoja wa Mikoa iliyovuka malengo ya makusanyo katika kipindi cha miezi 6 ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa kukusanya mapato zaidi ya asilimia 100.

About Alex

Check Also

index

Serikali Yawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri Zote Nchini Kuhakikisha Wanatokomeza Malaria

Na, Paschal Dotto- MAELEZO 22.10.2018 Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + seventeen =