Wednesday , April 24 2019

Home / MICHEZO / YANGA YAZIDI KUIPA PRESHA SIMBA MBIO ZA UBINGWA,YAANDIKA HISTORIA MJINI MTWARA

YANGA YAZIDI KUIPA PRESHA SIMBA MBIO ZA UBINGWA,YAANDIKA HISTORIA MJINI MTWARA

IMG_0390-640x427

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara  Timu ya Wananchi Yanga hatimaye imeandika historia katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara kwa kuondoka na Pointi tatu baada ya kuwafunga wenyeji Ndanda FC jumla ya magoli 2-1 Mchezo wa kiporo ikiwa ni kuhitimisha Mzunguko wa 19.
Msimu huu Yanga inaonekana kuwa ni ya kawaida kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota wao muhimu wa kikosi cha kwanza kuwa majeruhi licha ya hivyo imeendelea kuvunja mwiko kwa kupata ushindi kwenye viwanja vigumu ambapo mara nyingi huwa wanafungwa ama kupoteza mechi.
Alianza kiungo mshambuliaji Pius Charles Buswita kufunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi.

Beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy akaifungia bao la pili Yanga SC dakika ya 29 baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Ndanda kufuatia pasi ya Buswita
Yanga ingemaliza kipindi cha kwanza inaongoa kwa mabao 3-0 kama si kiungo Mkongo, Tshishimbi aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland kukosa penalti dakika ya 38, ambayo ilipanguliwa na kipa Jeremiah Kisubi kufuatia John Tibar George kuunawa mpira kwenye boksi.
Kipindi cha pili, Ndanda walibadilika na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa Yanga hadi kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi bao hilo lilifungwa na Nassor Kapama dakika ya 46 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa
Hadi Mwamuzi Florentina Zablon wa Dodoma anamaliza Mpira Yanga kwa mara ya kwanza wanatoka na pointi tatu na kuzidi kuwapa presha Simba katika mbio za Ubingwa huku wakifikisha jumla ya Pointi 40 tofauti ya tano na Kinara wa Msimamo Simba wakiwa na 45.

About Alex

Check Also

1

Wizara ya Habari yawasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/20

 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

thirteen + fifteen =