Mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara umechezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa kaitaba Stadium ambapo Kagera Sugar ilikuwa mwenyeji dhidi ya Mwadui FC.
Mchezo huo umemalizika kwa wenyeji Kagera Sugar kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuifanya ianze taratibu safari ya kuepuka kushuka daraja.
Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Japhet Makari kwenye dakika ya 26.
Matokeo hayo yameipandisha Kagera Sugar kutoka nafasi ya 14 mpaka ya 12 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 21.