Wednesday , December 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA ANASA WATU WANAOFANYA BIASHARA YA VIROBA VYA POMBE AMBAVYO VILISHAPIGWA MARUFUKU

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA ANASA WATU WANAOFANYA BIASHARA YA VIROBA VYA POMBE AMBAVYO VILISHAPIGWA MARUFUKU

1

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kushoto akimuonyesha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kibaha (OCD) Innocent Feksi baadhi ya viroba vya pombe aina ya Gin ambavyo vilikamatwa baada ya kufanyika kwa msako mkali katika baadhi ya maduka yaliyopo eneo la maili moja ambayo yanauza vileo  ambavyo viivyapigwa marufuku na serikai tangu mwaka jana.

2

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akionyesha waandishi wa habari hawapo pichani viroba vya pombe ambavyo vilibaika kuuzwa  kinymela katika baadhi ya maduka ya jumla ya vileo katika eneo la maili moja, baada ya kufanyika msako mkali na kuweza kubaini kuuza vinywaji hivyo ambavyo vilishapigwa marufuku.

3

Mmoja wa vijana wanaoishi katika eneo la maili moja Wilayani Kibaha amabaye akutaka jina lake litajwe akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Kibaha  Assumpter Mshama hayupo pichana jinsi ya virobo vilivyokuwa vinawaletea madhara  pindi walipokuwa wanavitumia

4

Baadhi ya umati wa vijana ambao walifurika kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha wakati wa msako huo wa kukagua maduka amabyo yanauza vileo ambavyo vimepigwa marufuku na serikali ya awamu ya tano

(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU

………………..

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

LICHA ya serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku uuzaji na utengenezaji  wa pombe aina ya viroba lakini imebainika kuwepo kwa  baadhi ya  wamiliki wa maduka katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani bado  wameamua kukaidi agizo hilo kwa kuamua kuendelea kuuza vinywaji hivyo kinyemela hali ambayo inahatarisha  usalama wa afya  zao kwa watumiaji hususan vijana.

Hali hiyo imebainika baada ya MKUU wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama  amefanya msako mkali wa kushitukiza katika baadhi ya maduka yanayouza vinjwaji vya jumla na rejareja na kuweza kubaini kuwepo kwa baadhibyao bado kuendelea kujiusisha na uuzaji wa pombe aina ya viroba ambavyo vilivyopigwa marufuku na serikali ya awamu ya tano.

Mkuu huyo katika kulikomoesha suala hilo ametoa onyo kali wa watu ambao watabainika kuhusika katika uuaji wa viroba watachukulia hatua kali a kisheria ikiwemo kulipa faini ili iwe fundisho kwa wengine  ambao wanakiuka agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

 

Katika hatua nyingine Mkuu huyo alitoa tamko la serikali ya Wilaya ya Kibaha endapo wakikuta eneo lolote ambalo linajihusiha na kuuza pombe mchana wakati wa kipindi cha muda wa kazi kinyume kabisa na sheria na taratibu watu ambao watahusika na kuwajibishwa watakuwa ni watendaji wa Kijiji  wote pamoja na watendaji wa mtaa.

Nao baadhi ya vijana ambao hawakutaka kutajwa majina yao  wametoa ushuhuda kutokana na madharaya kutumia viroba hivyo na kusema kuwa wameipongeza serikali kw akupiga marufuku vinywaji hivyo kwani  vilikuwa vinapoteza nguvu kazi ya vijana  na kukiri kuwepo kwa baadhi ya watu ambao bado wanaendelea kuviuza hivyo wameimba mamlaka inaohusika kuendelea kufanya msako mkali kwa lengo la kuwea kuhakikisha biashara hiyo aiendelei kufanyika tena.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa mwaka 2017 alipiga marufuku uuzaji wa pombe aina ya viroba vya aina mbali mbali,kutokana na kuleta mathara makubwa kwa watumiaji hususan kwa upande wa vijana,lakini cha kushangaza kuna baadhi ya  maduka katika  maeneo bado  yamebainika kuwa  yanaendelea kufanya biashara hiyo ya uuzaji wa viroba kinyemela na kukaidi agizo la serikali.

About Alex

Check Also

02

Wachuuzi wa Soko la Samaki Bagamoyo Wamuangukia Mbalawa

  Na.Stahmil Mohamed wachuuzi wa samaki katika soko la samaki wilayani bagamoyo wamemuomba waziri maji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 3 =