Thursday , January 17 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAGANGA WA TIBA YA ASILI WAOMBWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA KISHIRIKINA

WAGANGA WA TIBA YA ASILI WAOMBWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA KISHIRIKINA

DSC_1054

Na Florah Raphael.

Waganga wa tiba asilia nchini watakiwa kujiepusha Na matangazo yanayokinzana na sheria, kanuni na taratibu ikiwa ni pamoja na kuondoa mabango yanayoonyesha kuwa wanaweza kuponya magonjwa sugu kama vili Ukimwi na matangazo yenye kupotosha jamii na kuambiwa kuwa matangazo yote lazim yapate kibali kutoka baraza la tiba asili na tiba mbadala kabla ya kuyabandika sehemu yoyote au kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa Leo na naibu waziri wa afya, wazee, jinsia na maendeleo ya watoto, Faustine Ndugulile alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Leo jijini Dar es salaam, amesema kuwa tiba asili ni huduma rasmi za afya Tanzania kuanzia pale ilipojumuishwa katika Sera ya afya na kutungwa kwa sheria ya tiba asili na tiba mbadala namba 23 ya mwaka 2002 na mwaka 2005 baraza la tiba asili lilipoundwa kuwa chombo kikuu cha kusimamia shughuli zote za tiba asili.
Aidha amesema kuwa madhumuni ya sheria hiyo ni kusimamia, kudhibiti na kuendeleza tiba ya asili ya Tanzania pamoja na kudhibiti maadili ya uganga na ukunga wa tiba asili nchini na kuhakikisha kuwa unapewa kipaumbele  pia ameongeza kuwa sheria hiyo inalinda afya na haki za watumiaji wa tiba ya asili, kuboresha na kuendeleza dawa ya asili, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuwahimiza wananchi wasitoe wala kuuza dawa za asili kiholela.
Pia Ndugulile amesema kuwa wagangs woye nchini wanatakiwa kujisajili, kusajili wasaidizi wao, vituo pamoja na dawa hususan dawa zinazouzwa katika maduka ya dawa ya asili na kubainisha kuwa hadi desemba 2017 waganga 16,300, vituo 212 na dawa asili 5 zilisajiliwa na baraza la tiba ya asili na kusisitiza kwamba bado juhudi binafsi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa kila mganga anasajiliwa.
Lakini naibu waziri amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria inayosimamia masuala ya tiba asili bado Wapo waganga wasio waadilifu wanaokiuka sheria hiyo wakiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vya waganga wanaopotosha juu ya suala zima la usajili wa serikali jambo ambalo linapelekea kukwamisha watendaji wa serikali pindi wanapotimiza majukumu yao kwa kuwadanganya viongozi wa serikali kwa barua za kugushi kwa lengo la kupata ruhusa ya kusajili waganga na kuwaomba waache Mara moja kwani suala hill limeshapelekwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu.
Pia amesema kuwa serikali inawahamasisha waganga wote wa tiba asili kujiepusha na migongano ndani ya jamii kwa kutohusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa na kuwataka waganga hao kishirikiana katika kupanga mikakati ya kudhibiti na kuondoa kabisa vitendo vichafu vinavyochafua taaluma yao kama vile upigaji ramli, mauaji ya vikongwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, ukeketaji na vitendo vyote vinavyohusishwa na uchawi na ushirikina.

About Alex

Check Also

HA2

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini leo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

six + 16 =