Wednesday , December 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / WATANZANIA WATAKIWA KUPIMA UGONJWA WA MACHO ANGALAU MARA MOJA KWA MWAKA

WATANZANIA WATAKIWA KUPIMA UGONJWA WA MACHO ANGALAU MARA MOJA KWA MWAKA

DSC_1054

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa uma wakati akitoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam.

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari wakati akitoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam.

………………………..

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

WATANZANIA wametakiwa kujua afya zao hususan magonjwa yanayohusu macho angalau mara moja katika mwaka ili kuweza kutambua juu ya mustakabali wa macho yao. 

Hayo yamezengumzwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa   kutoa tamko katika wiki ya maadhimisho ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho Jijini Dar es salaam. 

“Wanaohathirika zaidi na Ugonjwa huu ni Barani Afrika na watu wenye umri kuanzia miaka 40 na kuendelea hivyo watanzania tujijengee mazoea ya kwenda kuangalia afya zetu hususani ugonjwa huu angalau mara moja kwa mwaka” alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa ugonjwa huo wa shinikizo la macho huambatana na kushindwa kuona mbali na dalili zake za mwanzo si rahisi kuziona kwa wakati huo. 

Kwa mujibu wa Dkt. Ndugulile amesema kuwa takribani watu  milioni1. 74 wana changamoto ya kutoona vizuri nchini Tanzania na bado haijakadiriwa ni mikoa gani hasa ina athari kubwa kwani ukusanyaji wa takwimu bado unaendelea. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa matibabu ya ugonjwa wa presha ya macho   yanapatikana katika hospitali zote za serikali nchini ikiwemo dawa pamoja na upasuaji kama utawahi mapema. 

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile alisistiza kuacha utumiaji ovyo wa vilevi, uvutaji sigara na badala yake kujikita kwenye ufanyaji wa mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kuepuka magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na mengineyo. 

Siku ya Ugonjwa wa presha ya macho itahadhimishwa kwa vituo vya afya kutoa huduma ya upimaji macho kuanzia tarehe 11 mpaka itapofikia kilele 17 machi 2018  na imebeba kauli mbiu   “OKOA UONI WA MACHO YAKO”. 

About Alex

Check Also

02

Wachuuzi wa Soko la Samaki Bagamoyo Wamuangukia Mbalawa

  Na.Stahmil Mohamed wachuuzi wa samaki katika soko la samaki wilayani bagamoyo wamemuomba waziri maji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 2 =