Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Yakutana na Mhe. Manyanya Mkoani Iringa

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Yakutana na Mhe. Manyanya Mkoani Iringa

1

Mashine mbalimbali za kusaga na kuboa mahindi zilizobuniwa na kutengenezwa na SIDO Iringa.

3

Moja ya tenki la kuchuja asali, tenki hili limebuniwa na wajasiriamali wa TEJO NATURAL HONEY na kutengezwa na Karakana ya SIDO Iringa.

4

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Ludovick Nduhiye akisalimiana na waheshimiwa wabunge mara baada ya kuwasili katika ofisi za SIDO ili kupokea taarifa iliyoandaliwa na SIDO Mkoa wa Iringa.

7

Makamu mwenyekiti wa kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Innocent Bashunga (mb) akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya SIDO Iringa, pembeni ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (mb)

9

Mkuu wa Karakana SIDO Iringa Mhandisi Nestory H. Ngoromela akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira.

14

Viti na bidhaa mbalimbali za mbao zilizo buniwa na kutengenezwa na wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.

18

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.

19

Baadhi ya wabunge wa kamati ya ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.

………………..

Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yakutana na Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na ku[pokea taarifa ya SIDO Iringa.

katika taarifa yao SIDO wameeleza shughuli mbalimbali wanazofanya hasa katika kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwapa elimu, mikopo yenye riba nafuu na ujuzi.

Baada ya kupokea taarifa hiyo kamati ya bunge ikiongozwa na makamu mwenyekiti Mhe. Innocent Bashunga (mb) ilitembelea eneo la SIDO Iringa na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa kiwandani hapo na kutembelea kiwanda cha Darsh ambacho pia walisaidiwa katika ubunifu wa baadhi ya mashine kiwandani hapo lakini pia SIDO ndio waliohusika katika ushawishi wa uanzishwaji wa kiwanda hiko ili kusaidia wakulima wa nyanya.

Kamati ya bunge imeishauri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kufanya juhudi kubwa kusaidia shirika hili la SIDO kwani ndio nguzo pekee kuelekea uchumi wa Viwanda, hivyo ni lazima kusaidiwa kupata teknolojia za kisasa ili kusaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani katika masoko ya kimataifa.

About Alex

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 + four =