Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI WA UJENZI WA NYUMBA 36 ZA JESHI LA POLISI MFIKIWA CHAKE CHAKE PEMBA

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI WA UJENZI WA NYUMBA 36 ZA JESHI LA POLISI MFIKIWA CHAKE CHAKE PEMBA

Q

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.

4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.

9

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.

11

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea mifuko ya saruji zaidi ya elfu sita kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Tanga Cement Bw.  Lawrence  Masha jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

…………………………………………………………………………………..

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu  Hassan amemtaka Mkuu wa  Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.

Kwa Upende wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi kufanya kazi kwa taratibu na sheria lakini pia alitoa wasihi kwa wanasiasa wanaochochea vurugu kwani wao watachukuliwa kama wahalifu na si wanasiasa.

Ziara ya Makamu wa Rais imekamilika leo ambapo pia alitembelea Hospitali ya Abdala Mzee ambapo alijionea vifaa vya kisasa vilivyowekwa na huduma bora zinazotolewa.

Makamu wa Rais pia aliweka mawe ya Msingi katika ujenzi wa madarasa katika skuli ya sekondari ya Ali Khamis Camp pamoja na ujenzi wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Ole.

About Alex

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three + 6 =