Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan azungumza na wananchi Mkoa wa Kaskazini Pemba

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan azungumza na wananchi Mkoa wa Kaskazini Pemba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Huduma ya Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kituo hicho cha Mama na Mtoto cha Shumba Vyamboni kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo jumla ya Wananchi 5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto chini ya umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe na ustawi wa mama na mtoto.

Vijiji vitakavyofaidika na huduma ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani na Bule.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhimiza shughuli za maendeleo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Bi. Mrashi ambapo alimkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake inayojengwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika eneo la Sizini.

Mwisho Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo aliwaambia wakina Mama kuwa mstari wa mbele katika kuonesha njia ya kuwa kiongozi bora.

About bukuku

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen + 19 =