Thursday , December 13 2018

Home / BIASHARA / AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO

AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO

2018-03-27-PHOTO-00000472
Hatimaye Kampuni ya Simu ya Airtel yawatendea haki wana Gairo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel.
Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Airtel ndio mkombozi mkubwa wa wananchi wa Gairo hasa vijijini. Bado mawasiliano  ya simu ni changamoto kubwa sana Gairo.  
Mhe. Mchembe aliendelea kuwapongeza Airtel kwa ajira zaidi ya 400 nchini kupitia ofisi zinazozinduliwa sasa. Vijana wa Gairo pia ni wafaidika wa Ofisi hizo.
Kabla ya kufunguliwa ofisi hizo, wananchi walikuwa wanaenda Dodoma au Morogoro kwa huduma mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa na Airtel wenyewe.
Mhe. Mchembe anayakaribisha mashirika mengine ya simu kufungua ofisi Gairo. Wilaya inakuwa kwa kasi kubwa na mzunguko wa pesa ni mkubwa na mawasiliano yanahitajika kwa kasi kubwa.
# Gairo Maendeleo Fasta kwa Mwendo Mdundo
# Hapakazitu

About Alex

Check Also

A 1-min

Tigo Wazindua Malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha

Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka akizungumza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × 5 =