Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

index

 

 

  • MTU MMOJA ANATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA NA YEYE MWENYEWE KUJINYONGA HADI KUFA WILAYANI MAGU.

 

KWAMBA TAREHE 26/03/2018 MAJIRA YA SAA 12:00HRS KATIKA KIJIJI CHA MAHAHA KITONGOJI CHA MWAMTAMBI KATA YA SHISHANI TARAFA YA NDAGALU WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN NTEMI, MIAKA 23, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MAHAHA, ANATUHUMIWA KUMUUA MKEWE AITWAYE CASTA EDWARD KWA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUFARIKI DUNIA KISHA NA YEYE MWENYEWE KUJINYONGA KWA KUTUMIA WAYA WA UMEME HADI KUFARIKI DUNIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INADAIWA KUWA WAWILI HAO WALIKUWA WAKIISHI PEKE YAO NA KABLA YA TUKIO HILO KUTOKEA WANANDOA HAO WALIKUWA WAKIISHI KWA AMANI NA UPENDO BILA MGOGORO WA AINA YEYOTE KATI YAO. LAKINI TAREHE NA MAJIRA TAJWA HAPO JUU BABA MWENYE NYUMBA WALIYOPANGA MAREHEMU AITWAYE DAUD PHILIPO ALIPITA MAENEO YA KARIBU NA NYUMBA YAO NDIPO ALIONA DAMU CHINI YA MLANGO KISHA ALIPOKWENDA KARIBU ALIGUNDUA MKE WA MPANGAJI WAKE AMEUAWA NDIPO ALITOA TAARIFA KWA MAJIRANI NA KITUO CHA POLISI.

POLISI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUKUTA MWILI WA MWANAMKE UKIWA MLANGONI NDANI YA NYUMBA NA ENEO LA TUKIO LIKIONESHA MIBURUZO YA DAMU TOKA CHUMBANI HADI MLANGONI HUKU MLANGO UKIWA UMEFUNGWA KWA KUFULI. VILEVILE POLISI WALIINGIA CHUMBANI NA KUUKUTA MWILI WA MWANAUME UKIWA UNANING’INIA KWA KUJINYONGA NA WAYA WA UMEME, WOTE WAWILI WAKIWA TAYARI WAMEPOTEZA MAISHA.

UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA MAUAJI HAYO YALITEKELEZWA USIKU WA TAREHE 25/03/2018 KWANI KIJIJINI HAPO KULINYESHA MVUA KUBWA SANA KIASI KWAMBA MAJIRANI WASINGEWEZA KUSIKIA KILICHOKUWA KIKIENDELEA NDANI KWA WAWILI HAO. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA FAMILI ZOTE MBILI KWA MSIBA MZITO WALIOUPATA, MWENYEZI MUNGU AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WANACHOPITIA. SAMBAMBA NA HILO PIA ANATOA WITO KWA WANANDOA WOTE KUWA PINDI MMOJA WAO ANAPOKOSEA JAMBO LOLOTE WAEPUKE TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA KISHERIA. PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

About Alex

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 + nineteen =