Monday , December 10 2018

Home / MICHEZO / Dulla Mbabe: Si Ngumi tu, Hata Soka Naweza

Dulla Mbabe: Si Ngumi tu, Hata Soka Naweza

1-7

Mchezaji wa timu ya Dame Boxing, Boxer, Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”(kulia) akikabiliwa na walinzi wawili wa timu ya Wakuvesha zote za Mwananyamala wakati wa Bonanza lililoandaliwa na Vijana CCM Tawai la Mwanjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam.Timu ya Wakuvesha ilishinda 2-1.

…………………………………………………………………………

Mwanamasumbwi , Abdallah Pazi( Dullah Mbabe) amebambwa kitaa akicheza Soka mitaa ya Mwananyamala katika Uwanja wa CCM Mwinjuma lililoandaliwa na Vijana wa CCM wa Tawi hilo mwishoni mwa wiki.

Katika Bonanza hilo, Dullah Mbabe alikuwa akichezea timu ya Dame Boxing akihudumu kama namaba tisa,ambapo katika mechi yao ya awali dhidi ya Wakuvesha walifungwa 2-1.

Mechi ya pili timu ya Dame Boxing ilicheza na timu ya Gereji ambapo timu ya Dame Boxing ilishinda 3-0, magoli mawili yalifungwa na Dullah Mbabe.

Akizungumza na mwandishi wetu, Dullah Mbabe alitamba kuwa mimi si Boxing tu bali hujumuika pia na ndugu na marafiki kufanya mazoezi ya mpira wa miguu, “Lakini leo tuna Bonanza hapa ambapo timu itakayoshinda inazawadiwa Mbuzi mmoja” alisema Dullah Mbabe.

Bonanza hilo lilijumuisha timu mbalimbali za mitaa ya Mwananyamala lengo ikiwa kuleta mshikamano kama Vijana wa eneo moja lakini pia kuhamasishana kufanya mazoezi kwani michezo ni afya, michezo huleta kufahamiana.

Dullah Mbabe kwa sasa anajiandaa na mpambano  wa IBF unaotarajia kufanyika Nchini China hivyo anatarajia kusafiri April 24, mwaka huu kueleke China.

About bukuku

Check Also

7178932-0-image-m-13_1544301930293

MESSI AFUNGA MABAO MAWILI BARCELONA YAICHAPA 4-0 ESPANYOL UGENINI LA LIGA

Lionel Messi akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona dakika za 17 na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − three =