Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / TBL Group yawaasa wanafunzi vyuo vikuu kuwa wabunifu, na kujiamini

TBL Group yawaasa wanafunzi vyuo vikuu kuwa wabunifu, na kujiamini

????????????????????????????????????

Meneja vipaji wa TBL Group na ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Lilian Makau   akitoa mada

????????????????????????????????????

Meneja   Uzalishaji wa Darbrew iliyopo chini ya TBL Group , Neema Arora,akitoa mada

????????????????????????????????????

Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo Vikuu wakimsikiliza kwa makini  Meneja wa Chapa za kampuni wa TBL Group , Amou Majok.

????????????????????????????????????

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group na wanafunzi  waliohudhuria wakifuatilia matukio.

………………………………………………………………….

-Pia watakiwa kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto za ajira na uthubutu wa kujiajiri
Taasisi na makampuni mbalimbali yameshiriki katika maonyesho na semina za kuwaandaa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu kuwandaa kuingia kwenye ajira pindi watakapomaliza masomo yao.Semina hiyo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali inavyotoa elimu ya juu.
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni yake mama ya ABIn Bev ilishiriki katika maonyesho hayo, ambapo Mameneja wake  waandamizi wakiongozwa na Meneja vipaji wa TBL Group na ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Lilian Makau  ,walitoa mada mbalimbali za kuwajengea uwezo wanafunzi kuwa wabunifu,kujiamini na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika  ajira.
Wanafunzi wengi pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu taratibu za ajira katika kampuni ya TBL Group,  walielezwa  kuwa kampuni inatoa fursa za ajira kwa watanzania wote na taratibu zake za ajira ziko wazi na pia kuwa imekuwa na utaratibu wa kuajiri wasomi waliohitimu mafunzo vyuoni na kuwapatia mafunzo ya ndani na wengi wao wametokea kuwa na utaalamu wa kiwango cha juu baada ya muda mfupi kwenye ajira zao.

About bukuku

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × five =