Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / VERTIV YAJA NA VIFAA VYA KISASA VYA KUKABILIANA NA MAJANGA YA UMEME

VERTIV YAJA NA VIFAA VYA KISASA VYA KUKABILIANA NA MAJANGA YA UMEME

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 
KAMPUNI ya
Vertiv imefanya maboresho ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(Tehama) vinavyotumika katika ujenzi, viwandani na maofisini kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao
wamiliki wa viwanda na kampuni mbalimbali katika nchi za Afrika
Mashariki.
Akizungumza
jana Dar es Salaam, katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Rais  wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John
Wyk alisema kuwa wamefanya maboresho ya bidhaa zao ili kusaidia wateja wao
kujua endapo vifaa vyao vimepata hitilafu au la.
Amesema
bidhaa wanazozizalisha ni pamoja na vifaa vya kudhibiti nguvu ya umeme, Ac
zinazotumika kwenye viwanda, UPS na ambazo zimewekewa uwezo wa kutoa taarifa
kwa mtumiaji  kama kifaa anachotumia
kimeshindwa kufanya kazi kwa sababu gani.
‘’Tumefanya
maboresho kwa bidhaa zetu ambapo wenye vituo vya data kama vile kampuni za
simu, ofisi za serikali na kampuni binafsi watapata taarifa kuonesha kuwa kama
UPS au AC za viwandani hazifanyi kazi kwa sababu ya umeme mdogo au kuna tatizo
lingine ambalo linapaswa kufanyiwa marekebisho,’’ amefafanua Wyk.
Amesisitiza
kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hizo ambazo zinatumika katika nchi za Jumuiya
ya Afika Mashariki (EAC) na Ulaya kwa kuwa wanaamini ukuaji wa teknolojia
unasaidia katika kuleta maendeleo chanya kwa kila nchi.
Naye
mshirika wa kibiashara na Mtaalamu wa masula ya mawasiliano, Mihayo Wilmore
amesema kuwa uboreshaji wa vifaa hivyo utasaidia maeneo mengi ikiwemo
hospitalini na maofisini ambako matumizi makubwa ya teknolojia hufanyika.
Amesema kuwa
watu wanaotumia mitambo mbalimbali katika shughuli zao, ni muhimu kujua ni muda
gani vifaa vyao vimeweza kuzimika kwa sababu ya kuisha kwa umeme, hutupata
ujumbe mfupi wa maandishi kuelezea tatizo lililotokea.
‘’Ni muhimu
kwa hospitali kujua UPS wanayotumia inaweza kuzimika kwa muda gani na sababu
gani zinazosababisha jenereta kuzimika
hii itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma haraka. Pia wameonesha uwezo
wa kutengeneza vituo vya data katika simu au kompyuta ili kutoa taarifa kwa
haraka kwa wateja wao,’’ ameeleza Wilmore.

 Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk  akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake katika soko la Tanzania Chini ya usambazaji wa kampuni ya Elcom Solution 

  Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano  kutoka  Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, Johan Terblanche akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake juu ya umuhimu wa UPS kutoka Vertiv katika Data Centre. 

 Mkurugenzi wa huduma  wa Vertiv Mashariki  ya Kati , Pascal Bodin akieleza namna kampuni hiyo ilivyoweza kunufaisha Viwanda vya ukanda huo.

 Mshirika
wa kibiashara
 wa  Elcom Solution  ambao wamewakaribisha Vertiv nchini, Mihayo
Wilmore akieleza Waandishi wa Habari umuhimu wa mitambo ya Vertiv katika sekta ya Afya nchini.

 Wakurugenzi  wa EL- COM Solutions , Deen Nathwani, Jimy Apson  na Amin Valji wakizungumza jambo wakati wa Warsha wa kutambuslisha bidhaa za Vertiv nchini.

Wafanyakazi wa Vertiv wakiwa katika picha ya pamoja na Washirika wao El-com Solution na washirika wengine kutoka nchini Kenya mara baada ya kumaliza warsha ya kutambulisha bidhaa zao Tanzania 

About Alex

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 + 1 =