Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA IRAN.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA IRAN.

V25A0044

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (wa pili kulia), Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (kulia) na Afisa kutoka ubalozi wa Iran nchini Tanzania Ndg. Maisara Ally (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

V25A9917

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (wa pili kulia), ugeni kutoka Bunge la Iran ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.  Kulia ni Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang na Afisa kutoka ubalozi wa Iran nchini Tanzania Ndg. Maisara Ally (wa pili kushoto)

V25A9973

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian

V25A0138

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu akiongoza mazungumzo baina ya wajumbe wa kamati hiyo na Wabunge kutoka Bunge la Iran, walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (wan ne kulia) na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mousa Frahang (watatu kulia) leo katika ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.

V25A9857

Ugeni kutoka Bunge la Iran ulioongozwa na  Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (katikati), Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (wa pili kulia)wakifuatilia kikao cha Bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma. Wengine ni Wabunge na Maafisa kutoka Bunge la Iran

V25A9871

Ugeni kutoka Bunge la Iran ulioongozwa na  Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (katikati), Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (wa pili kulia)wakifuatilia kikao cha Bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma. Wengine ni Wabunge na Maafisa kutoka Bunge la Iran

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

About bukuku

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × one =