Monday , October 22 2018

Home / MICHEZO / BAADA YA KUSAINI MKATABA NA YANGA KOCHA MPYA ATEMA CHECHE KUELEKEA DERBY YA KARIAKOO

BAADA YA KUSAINI MKATABA NA YANGA KOCHA MPYA ATEMA CHECHE KUELEKEA DERBY YA KARIAKOO

KOCHA

Baada ya kusaini Mkataba wa kuitumikia Yanga mapema leo, kocha mpya wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Mwinyi Zahera ameelekea Morogoro kuungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi mkoani humo.

Kocha Zahera amesaini mkataba wa miaka miwili na  ametaka kuanza kazi mara moja hasa baada ya kuelezwa Jumapili ijayo kutakuwa na ‘derby’ dhidi ya Simba mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa

“Tutazungumza na uongozi wa Yanga, lakini nadhani nitaanza kazi mara moja,” amesema.

Akizungumzia kuhusu mchezo wake wa kwanza kuwa dhidi ya Simba, Zahera amesema hilo halimtii hofu kwa kuwa ameongoza michezo ya aina hiyo mingi.

“Nimekuwa kocha kwenye nchi za Afrika na Ulaya, nimeongoza michezo ya aina hiyo mingi sana, hao Simba waje tu,” amesema Zahera anayeweza kuzungumza lugha ya kiswahili kwa kiwango cha kuridhisha.

About Alex

Check Also

Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kwenye maziko ya msanii mwezao Mashaka jana.

RIDHIWANI KIKWETE AUNGANA NA WASANII KUMZIKA MASHAKA

Na Shushu Joel,Dar MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 + ten =