Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA SOKO KUU LA KIBAIGWA

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA SOKO KUU LA KIBAIGWA

V25A1242

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipatiwa maelezo na  Meneja wa Soko la kibaigwa Ndg. kusekwa Dalali wakati wa ziara yake ya kutembelea soko la kibaigwa na kuangalia changamoto Mbali mbali zinazopatikana katika soko hilo lililopo Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma.

V25A1247

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Fundi Mitambi wa soko la kibaigwa  Ndg. Omary Salmin wakati wa ziara yake ya kutembelea soko la kibaigwa ilifanyika hivi karibuni Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma.

V25A1764

Makamu Mwenyekiti kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Mwanne Nchemba (katikati) akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo, Viongozi kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kibaigwa leo kikao kilichofanyika Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Josephat kandege na Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), Ndg. Stephen Ruvuga (kulia)

V25A1920

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Josephat kandege (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo, Viongozi kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kibaigwa leo kikao kilichofanyika Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma. Katikati ni Makamu Mwenyekiti kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Mwanne Nchemba na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), Ndg. Stephen Ruvuga (kulia)

V25A1644

Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Angelina Malembeka akizungumza wakati wa kikao cha pamoja  baina ya kamati hiyo ya Bunge, Viongozi kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) na Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kibaigwa leo kikao kilichofanyika Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma.

V25A1333

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipatiwa maelezo na  Meneja wa soko la kibaigwa Ndg. Kusekwa Dalali wakati wa kukagua mizani iliyopo katika soko la kibaigwa katika ziara yake ya kutembelea miundo mbinu ya soko hilo katika soko hilo lililopo Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma.

V25A1981

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Josephat kandege (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Mwanne Nchemba (wa pili kulia waliokaa) na Viongozi kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) walioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Stephen Ruvuga (kushoto waliokaa) na Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kibaigwa leo Wilayani kibaigwa Mkoani Dodoma.

V25A1439

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa Mwanne Nchemba (hayupo kwenye picha) wakati wa majadilianao baina ya kamati hiyo na Viongozi kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE

About Alex

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − three =